MGALU AWATAKA TANESCO NA REA KUJITATHMINI

Naibu Waziri wa Nishati, Subira Mgalu amewataka watendaji wa Wakala wa Nishati Vijijini (REA) na Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO) kujitathmini katika kazi ya upangaji wa Vijiji vinavyosambaziwa umeme nchini ili kuepusha migogoro kati ya Serikali na wananchi. Naibu Waziri ametoa agizo hilo alipokua katika Kijiji cha Matai, Wilayani Kalambo Mkoa wa Rukwa wakati akikagua kazi ya usambazaji umeme ambapo alikua ameambatana na Naibu Waziri wa Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI), Josephat Kandege ambaye pia ni Mbunge wa Jimbo la Kalambo. Aidha amesema amesikitishwa…

Soma Zaidi >>

HATIMAYE ZITTO KABWE AHUTUBIA TARIME, ATUMIA JUKWAA LA NCCR-MAGEUZI KUOMBA KURA ZA CHADEMA

Na John Marwa@darmpya.com Tarime Mbunge wa Jimbo la Kigoma Mjini na Kiongozi wa Chama cha Act Wazalendo Mhe. Zitto Zuberi Kabwe Leo amefanikiwa kufanya mkutano wa hadhara wa kumnadi mgombea wa udiwani kata ya Turwa Mjini Tarime, Charles Mnanka baada ya jana kushindwa kufanya mkutano huo kwa madai ya kuekewa zuio na Mtendaji wa kata hiyo. Inadaiwa kuwa, zuio hilo lilikuja mara baada ya mgombea wa Chama cha Mapinduzi (CCM) Chacha Ghati Mwita kukituhumu Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) kutumia lugha za matusi kwenye kampeni mwanzoni mwa wiki hii.…

Soma Zaidi >>

MAVUNDE: KILELE CHA SIKU YA VIJANA DUNIANI KUFANYIKA KITAIFA MKOANI ARUSHA

Naibu Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu Kazi,Vijana na Ajira Mh Anthony P. Mavunde ameeleza kwamba Serikali itaendelea kuweka mazingira wezeshi kwa vijana kustawi kijamii,kisiasa na kiuchumi. Kauli hiyo ameitoa mapema leo wakati akizungumza na waandishi wa habari kuhusu maadhimisho ya Kilele Siku ya Vijana Duninia Kitaifa yatafanyika mkoani Arusha tarehe 12.08.2018 ambapo kauli mbiu ya mwaka huu MAZINGIRA SALAMA KWA VIJANA “Natoa wito kwa vijana wote nchini, wazazi na wadau wa Vijana washerehekee siku hii muhimu ili kwa pamoja tuonyeshe na kutambua umuhimu wa vijana kama washiriki wa…

Soma Zaidi >>

FREDDY LOWASSA ACHUKUA FOMU YA KUGOMBEA UBUNGE JIMBO LA MONDULI

ARUSHA. Mtoto wa Waziri Mkuu Mstaafu, Edward Ngoyai Lowassa, aitwaye Freddy Edward Lowassa, amechukua fomu ya kuomba ridhaa ya kugombea ubunge Jimbo la Monduli mkoani Arusha, na kuwa miongoni mwa wanachama watano wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) waliochukua fomu, baada ya aliyekuwa mbunge wa jimbo hilo, Julius Kalanga alijiuzulu na kujivua uanachama wa Chadema na kuhamia CCM. Akizungumza na Mtandao wa Darmpya.com leo Agosti 9, Katibu wa CHADEMA Kanda ya Kaskazini, Mheshimiwa Aman Golugwa amesema Fred amechukua fomu na kurejesha. Mbali na hivyo, Golugwa ambaye pia ni Mwenyekiti…

Soma Zaidi >>

WALICHOZUNGUMZA RAIS MAGUFULI NA MUSEVENI HII LEO

Rais wa Uganda Yoweri Kaguta Museveni amewasili Nchini Tanzania kwa ziara ya kikazi ya siku moja na kupokelewa na mwenyeji wake Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli, ambapo wamefanya mazungumzo yanayohusu ushirikiano na Maendeleo kati ya nchi Afrika Mashariki. Museveni ambae ni mwenyekiti wa Jumuiya ya Afrika Mashariki, amesema ameshiriki mkutano wa Jumuiya ya Nchi zinazoibukia kiuchumi (BRICS) hivyo amewataka wafanyabiashara wa jumuia hiyo kuangalia uwezekano wa kuwekeza katika ukanda wa Afrika Mashariki ili kusaidia maendeleo ya wakazi wake. Ameongeza kuwa,Tanzania na Uganda ni…

Soma Zaidi >>

WALICHOZUNGUMZA RAIS MAGUFULI NA MUSEVENI HII LEO

DAR-ES-SALAAM. Rais wa Uganda Yoweri Kaguta Museveni, amewasili nchini Tanzania kwa ziara ya kikazi ya siku moja na kupokelewa na mwenyeji wake Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli, ambapo wamefanya mazungumzo yanayohusu ushirikiano na Maendeleo kati ya nchi Afrika Mashariki. Museveni ambae ni mwenyekiti wa Jumuiya ya Afrika Mashariki, amesema ameshiriki mkutano wa Jumuiya ya Nchi zinazoibukia kiuchumi (BRICS) hivyo amewataka wafanyabiashara wa jumuia hiyo kuangalia uwezekano wa kuwekeza katika ukanda wa Afrika Mashariki ili kusaidia maendeleo ya wakazi wake. Ameongeza kuwa, Tanzania na…

Soma Zaidi >>

RAIS DKT JOHN MAGUFULI AONGOZA MAMIA YA WAOMBOLEZAJI

RAIS wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt,John Magufuli aongoza mamia ya waombolezaji katika kuuaga mwili wa Marehemu Amri Athuman maarufu (King Majuto ) katika viwanja vya KARIMJEE Jijini Dar es Salaam. Msiba huo umehudhuriwa na Viongozi mbalimbali wa Serikali akiwemo Rais mstaafu wa awamu ya nne Dkt, Jakaya Kikwete, Viongozi wa Dini wakiongozwa na Mufti wa Mkuu wa Tanzania Sheikh, Abubakar Zubeir pamoja wasanii maarufu akiwemo Jacob Steven (JB). Akitoa salamu za pole kwa niaba ya Serikali Naibu Waziri wa habari Sanaa Utamaduni na michezo Juliana Shonza amesema kuwa,…

Soma Zaidi >>

NAIBU WAZIRI WA NISHATI, AWASHA UMEME MWAZYE

Naibu Waziri wa Nishati, Subira Mgalu amewasha umeme katika Kijiji cha Mwazye wilayani Kalambo Mkoani Rukwa. Katika uzinduzi huo ulihudhuriwa na Naibu Waziri wa Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI), Josephat Kandege, ambaye pia ni Mbunge wa Jimbo la Kalambo. Naibu Waziri wa Nishati, amemuagiza mkandarasi anayesambaza umeme katika Kijiji hicho, kutoondoka katika eneo hilo mpaka atakapomaliza kuunganishia umeme kwa  wananchi.

Soma Zaidi >>

RC ALLY HAPI :MARUFUKU BODABODA NA BAJAJI KUNYANYASWA IRINGA

Mkuu wa mkoa wa Iringa Ally Hapi amepiga marufuku kusikia vijana wa Boda Boda na bajaji katika mkoa huo kunyanyaswa na askari au Sumatra. Agizo hilo amelitoa leo wakati kikao chake  na viongozi wa bodaboda na bajaji mkoa wa Iringa . Kitika kikao hicho kilichoshirikisha viongozi wa jeshi la polisi ,maofisa wa Manispaa ,Sumatra na wakuu wa wilaya ya Iringa na Kilolo ,Mkuu huyo wa mkoa alisema ni wajibu wa viongozi wa serikali kusikiliza na kutatua kero za bajaji na bodaboda na sio viongozi kuwa kero kwa vijana hao. “Sitataka…

Soma Zaidi >>

MSANII MAGUMASHI ALIYEZUIWA NA MAREHEMU KING MAJUTO ASIUZE FIGO APATE PESA ,ATAKA STEVIN NYERERE ASITENGWE

Msanii Erasto  Kilowoko a.k.a Magumashi Msanii Erasto  Kilowoko a.k.a Magumashi  kushoto  akiwa na Dkt  Mduba  akiomboleza  msiba wa King Majuto  akiwa  Iringa. IKIWA leo  Rais  wa jamhuri ya  muungano wa Tanzania Dkt  John Magufuli amewaongoza  watanzania  katika kuaga  mwili  wa  msanii mkongwe na maarufu nchini Tanzania na Afrika Mashariki Amri Athuman maarufu King  Majuto   ,msanii  wa   vichekesho  mkoani Iringa Erasto Kilowoko a.k.a Magumashi ambae  alikatazwa na marehemu  King Majuto  kuuza  figo  yake amlilia mzee Majuto na  kuomba   wasanii  wasimtenge mwenyekiti wa wa Klabu ya Bongo Movie Unity, Steven Mengere  Nyerere…

Soma Zaidi >>