WANATAKA KUABUDIWA WANASAHAU KWAMBA BINADAMU HAWEZI KUWA MUNGU, RODRIGO DUTERTE AMECHELEWA KUFUATA NYAYO ZA MBABE NAPOLEON BONAPARTE.

Toleo la II. Vituko vya Rodrigo Roa Duterte mapema sana tarehe 10/6/2018 akiwa yupo Korea ya Kusini akiwahutubiaa wafilipino waishio Korea Kusini alifanya jambo ambalo liliwashangaza wengi sana duniani kotoe, Rodrigo Roa Durtete amewahi kushutumiwa na mashirika yanayotetea haki za binadamu katika kuwanyanyasa na jinsi anavyo wachukuliaa wanawake huko Ufilipino, akiwa Korea Kusini alimwita msichana mmoja wa kifilipino na kumwambia amkumbatie na baadae kumshawishi ampige busu la mdomoni mbele ya umati wa watu bila kujali alikuwa mke wa mtu au lah, lakini mwanamke yule akawa anasita sita na baadae akakubali…

Soma Zaidi >>

RAIS AFANYA MABADILIKO YA UONGOZI SERIKALINI, JERRY MURO, JOKATE MWEGELO WALA SHAVU

Jioni ya leo Julai 28, 2018, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli amefanya mabadiliko katika baadhi ya nafasi za uongozi serikalini.  Orodha hii hapa chini ni baadhi tu ya walioteuliwa: Jokate Mwegelo ameteuliwa kuwa Mkuu wa Wilaya ya Kisarawe mkoa wa Pwani Jerry Muro ameteuliwa kuwa Mkuu wa Wilaya ya Arumeru mkoa wa Arusha. Patrobas Katambi ameteuliwa  kuwa Mkuu wa Wilaya ya Dodoma. David Kafulila ameteuliwa kuwa Katibu Tawala wa Mkoa wa Songwe. Moses Machali ameteuliwa kuwa Mkuu wa Wilaya ya Nanyumbu mkoa wa…

Soma Zaidi >>

MAHAKAMA KUU YA TANZANIA YAWAKINGIA KIFUA MADIWANI CUF, LIPUMBA NA WENZAKE WAANGUKIA PUA

TANGA. Mbele ya Mheshimiwa Jaji Benhajj Masoud, Mahakama Kuu kanda ya Tanga, imetoa Amri ya kumzuia Mwenyekiti wa chama cha Wananchi (CUF), Prof. Ibrahim Limpumba, Magdalena Sakaya (Mb), pamoja na Halmashauri ya Jiji la Tanga na Mamlaka zingine zote ikiwemo NEC, kutoendelea na hatua zozote za kutaka kutangaza uwepo wa nafasi wazi za Udiwani kutokana na madai ya kuwavua Uanachama Madiwani. Maamuzi hayo yalitolewa hapo juzi Alhamisi Julai 26, mbele ya Mawakili wa jiji na Mwanasheria Mkuu wa Serikali kufuatia maombi madogo [Miscellenous Civil Application No. 30 of 2018], yaliyowasilishwa…

Soma Zaidi >>

WAZIRI LUKUVI APIGA MARUFUKU NYUMBA KUWEKEWA ALAMA YA ‘X’

DAR ES SALAAM. Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Wiliam Lukuvi, amepiga marufuku uwekaji wa alama ya ‘X’ kwenye makazi ya wananchi waliojenga katika maeneo ambayo hayajarasimishwa kote nchini. Waziri Lukuvi, ametoa kauli hiyo hapo jana Julai 27, 2018, jijini Dar es Salaam, alipokuwa akizungumza na waandishi wa habari wakati wa mkutano wa wadau wa ardhi waliokutana kujadili Mpango mji wa miaka 20 wa Jiji la Dar es Salaam. Mhe. Lukuvi alisisitiza kuwa, hakuna mwananchi atakayevunjiwa nyumba yake kwa sababu amejenga katika eneo ambalo halijarasimishwa, kwa sababu Serikali…

Soma Zaidi >>

WAITARA AJIVUA GAMBA CHADEMA.

NA TATU TAMBILE LEO tarehe 28, July, 2018 Mbunge wa Jimbo la Ukonga Jijini Dar es Salaam kupitia tiketi ya CHADEMA Mwita Mwikabe Waitara amejivua uanachama wa CHADEMA na kuamua kurudi CCM rasmi. Hayo yamejiri katika ofisi ndogo ya Makao Makuu CCM ambapo Katibu Mwenezi wa CCM Humphrey Polepole alimtambulisha Mwaitare mbele ya waandishi wa habari kuwa mwanachama rasmi wa chama hicho. Waitara amesema kuwa toka mwaka 2008 alikuwa  mwanachama wa CHADEMA  na kuchaguliwa kuwa mwenyekiti wa chama hicho na baadae mwaka 2015 akachaguliwa kuwa Mbunge wa Jimbo la Ukonga…

Soma Zaidi >>

DKT KAFULILA AWACHANA WAPINZANI IRINGA ASEMA HAKUNA ZAIDI YA CCM

kada maarufu wa chama cha NCCR Mageuzi Dkt David Kafulila amewashukia wapinzani nchini Tanzania kuwa ni wapinga maendeleo na kuwa CCM ni jibu la maendeleo kwa Taifa. Akimnadi mgombea wa CCM udiwani kata ya Mwangata Leo Kafulila kasema kuwa kazi kuwa inayofanywa na CCM nchini upinzani itapata shida sana kuweza kushinda. Alisema kuwa ufisadi ambao ulikuwa ukifanyika awali sasa chadema hawawezi kufurukuta .

Soma Zaidi >>

WAITARA KUTATUA KERO YA FIDIA YA MALIPO MRADI WA RELI YA KISASA ENEO LA GONGO LA MBOTO

G/MBOTO-UKONGA, DAR ES SALAAM. Mbunge wa Jimbo la Ukonga, Mheshimiwa Mwita Waitara (CHADEMA), ameahidi kuwatafuta viongozi wa Mamlaka ya Reli nchini (TRL) pamoja na Wizara ya Uchukuzi na Mawasiliano, kuwakutanisha na wakazi na wafanyabiashara wa kata ya Gongo la Mboto jijini Dar es Salaam, ili kumaliza mgogoro wa fidia unaotokana na Mradi wa Reli ya Kisasa ya Standard Gauge uliopita katika eneo hilo. Mh Waitara ameyasema hayo jana Julai 27, katika ziara yake ya kutembelea wananchi waliompigia kura ndani ya eneo lake la uwakilishi, katika kata hiyo, ambapo alikwenda kuwapa…

Soma Zaidi >>

MBUNGE NYAMAGANA AELEZA JINSI SERIKALI YA CCM ILIVYOTIMIZA AHADI ZAKE, ATAJA UJENZI WA BARABARA NA UBORESHAJI MAZINGIRA

Mbunge wa Jimbo la Nyamagana (CCM) Mhe. Stanslaus Mabula amebainisha utekelezaji wa ahadi mbalimbali zilizotolewa na serikali jimboni humo, ambapo ametaja baadhi ya ameneo amabyo tayari ahadi zake zimekwisha kamilika kuwa ni pamoja na ujenzi wa barabara, ujenzi wa matundu ya vyoo, pamoja na uboreshaji wa sekta ya afya. Mhe. Mabula ameyasema hayo mapema siku ya jana Julai 27, 2018 alipokuwa akizungumza na wananchi wa kata ya Igogo ikiwa ni sehemu ya mwendelezo wa ziara yake katika kata 18 za Halmashauri ya Jiji la Mwanza, kukagua miradi ya maendeleo pamoja…

Soma Zaidi >>

SIFO KUWAKUTANISHA VIJANA NA VIONGOZI HALMASHAURI YA MKURANGA

Shirika lisilo la kiserikali la Social Information and  Facilitation Organisation (SIFO), linalofadhiliwa na foundation for civil society limewakutanisha vijana na viongozi wa Halmashauri ya wilaya ya mkuranga Mkoa wa Pwani ili kujadili mipango kazi kwa lengo la kukabiliana na changamoto  wanazokumbana nazo vijana katika Nyanja za elimu, uchumi pamoja na siasa. Mwenyekiti wa Halmashauri ya mkuranga Juma Abeid alisema serikali imejipanga vizuri kukusanya pesa za kusaidia vijana  walio katika jamii na kutoa elimu ili kila watakalolifanya wafanye kwa maarifa. Abeid aliyasema hayo alipokuwa Mgeni rasmi kwenye jukwaa la kuwasilisha changamoto…

Soma Zaidi >>

KAMPENI ZA UDIWANI IRINGA MJINI,CHADEMA NA CCM KUZINDUA MTAA MOJA LEO

KAMPENI ZA UDIWANI IRINGA MJINI VYAMA vya Chadema na CCM wilaya ya Iringa mjini leo kuzindua kampeni zake za udiwani katika mtaa na  kata moja ya Mwangata. Wakati chadema wakitegemea kufanya uzinduzi wao eneo la Mwangata B kuanzia saa nane mchana hadi saa 12 jioni ,CCM wanategemea kuzindua kampeni zao kwenye viwanja vya Isoka ofisi ya mtendaji wa kata. Taarifa ya Chadema iliyotolewa na mratibu kampeni chadema Leonce Marto inasema kampeni za Chadema kumnadi mgombea wa udiwani kata hiyo zitazinduliwa na mwenyekiti wa Chadema kanda ya Nyasa Mchungaji Peter Msigwa…

Soma Zaidi >>