DIWANI CHADEMA NYALUMBU AUMBUKA MBELE YA MBUNGE,MWENYEWE AJIBU MAPIGO

Mbunge wa jimbo la Kilolo Venance Mwamoto (kushoto) akipokea mic kutoka kwa diwani wa kata ya Nyalumbu kupitia Chama cha Chadema David Mfugwa leo kitongoji cha Dinginayo. ……………………………………………… WANANCHI wa kitongoji cha Dinginayo kata ya Nyalumbu wilayani Kilolo mkoani Iringa wamemshukia mbele ya mbunge diwani wao wa chadema cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) David Mfugwa kwa kukiuka taratibu za uitishaji wa mikutano na kufanya mikutano ya kisera kupitia redio. Wakizungumza katika mkutano wa mbunge wa jimbo la Kilolo Venance Mwamoto leo mara baada ya diwani huyo Mfugwa kuwatuhumu wananchi kuwa…

Soma Zaidi >>

MBUNGE WA NYAMAGANA AIMWAGIA SIFA SERIKALI AWAMU YA TANO KWA MIRADI YA MAENDELEO

Mbunge Jimbo la Nyamagana Mhe Stanslaus Mabula ameendelea na ziara yake ya kuwatembelea wananchi jimboni humo ili kubaini kero zao mbalimbali, na kukagua miradi ya maendeleo ambayo imekwisha tekelezwa mpaka kufikia hivi sasa. Siku ya leo Julai 25, 2018, Mhe. Mabula ametembelea kata ya Kishiri ambapo pamoja na mambo mengine amekagua maendeleo ya ujenzi wa Daraja la Kanido Sawah ambalo litagharimu shilingi Milioni 189 hadi kukamilika kwake. Akizungumza kwenye ukaguzi huo, Mhe. Mabula ameshukuru serikali ya CCM chini ya uongozi wa awamu ya tano ya  Mhe. Dkt. John Pombe Joseph Magufuli…

Soma Zaidi >>

KESI YA AKINA MBOWE YAPIGWA KALENDA HADI JULAI 31

Kesi inayowakabili viongozi tisa (9) wa CHADEMA akiwemo mwenyekiti wa chama hicho Freeman Mbowe, imepigwa kalenda hadi tarehe 31 Julai 2018 ambapo inatarajiwa kusomewa maelezo ya awali (Ph) katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu, jijini Dar es Salaam. Uamuzi huo umetangazwa hii leo Julai 25, 2018 mbele ya Hakimu Mkazi Mkuu, Wilbard Mashauri baada ya Wakili wa Serikali, Faraja Nchimbi kuomba Mbowe na wenzake  wapangiwe tarehe nyingine kwaajili ya kusomewa maelezo ya awali. Akifafanua kuhusu ombi lake hilo, Nchimbi amedai kuwa hatua hiyo inakuja kwa sababu mnamo siku ya tarehe…

Soma Zaidi >>

TAHADHARI: TAREHE 27 JULAI KUSHUHUDIWA TUKIO LA KUPATWA KWA MWEZI KWA MUDA MREFU ZAIDI

Taarifa kutoka kwa Shirika la Usimamizi wa Anga za Juu (NASA) zinasema kuwa siku ya kesho kutwa Julai 27, 2018, dunia itashuhudiwa tukio la kupatwa kwa mwezi, ambalo si la kawaida. Kwa mujibu wa habari iliyoripotiwa na BBC mapema siku ya leo inasema kuwa, shirika hilo limetoa taarifa inayosema tukio la kupatwa kwa mwezi mnamo siku hiyo ya Julai 27 litakuwa la muda mrefu zaidi kuwahi kutokea katika karne ya 21. Taarifa hiyo inaeleza kuwa tukio hilo litashuhudiwa kwa ukaribu zaidi katika maeneo ya Ulaya, Afrika, Mashariki ya Kati, katikati mwa…

Soma Zaidi >>

JEAN-PIERRE BEMBA KUGOMBEA URAIS NCHINI KONGO BAADA YA KUACHIWA HURU NA ICC

KINSHASA, DR CONGO. Kiongozi wa DRC na mbabe wa zamani wa kivita, aliyewahi kuwa Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo, Jean Pierre Bemba, baada ya mwezi uliopita kufutiwa mashitaka ya uhalifu dhidi ya binadamu na uhalifu wa kivita na Mahakama ya Kimataifa ya ICC, anatarajiwa kurejea nyumbani mwezi Agosti na kugombea urais nchini humo. Taarifa kuhusu Bemba kurejea Kongo, imetolewa na Eve Bazaiba, Katibu Mkuu wa chama kikuu cha upinzani cha Movement for the Liberation of Congo (MLC). Katika tangazo lililotolewa na chama hicho limefahamisha kuwa Bemba…

Soma Zaidi >>

MBUNGE VENANCE MWAMOTO APOKELEWA KWA SHANGWE KATA YA NYALUMBU AMBAYO DIWANI WAKE WA CHADEMA

MBUNGE wa jimbo la Kilolo mkoani Iringa Venance Mwamoto mchana huu amepokelewa kwa maandamano makubwa ya bodaboda kata ya Nyalumbu inayoongozwa na Diwani wa chadema cha Demokrasia na maendeleo (CHADEMA) David Mfugwa. Mbunge Mwamoto anaendelea na ziara yake ya kikazi ya kutembelea na kufanya mikutano ya hadhara katika kata  mbali mbali za jimbo hilo na Leo ni zamu ya vijiji vya kata ya Nyalumbu Akiwa katika kitongoji cha Luhanzo ameahidi kusaidia mashine ya kusaga ili kuondoa kero ya wanawake kutembea umbali mkubwa kufuata huduma ya mashine. Wakati kijiji cha  Ikuvala…

Soma Zaidi >>

KUENDANA NA KASI YA KANGI LUGOLA, MAGEREZA WAFANYA MABADILIKO KADHAA.

Ikiwa ni katika kuboresha utendaji kazi wa Magereza nchini, Kamishna Jenerali mpya wa Jeshi la Magereza, Phaustine Martin Kasike amefanya mabadiliko kwa Wakuu wa Magereza wa Mikoa na Vituo vingine vya Magereza hapa nchini. Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa siku ya jana Julai 24, 2018 na Mrakibu Msaidizi wa Magereza, Lucas Mboje imetaja mabadiliko hayo kuwa yanajumuisha aliyekuwa Mkuu wa Magereza Dodoma, Naibu Kamishna wa Magereza (DCP), Julius Sang’udi ambaye amehamishiwa Makao Makuu ya Magereza kuwa Mkuu wa Kitengo cha Huduma za Wafungwa, ambapo nafasi yake imechukuliwa na aliyekuwa Mkuu…

Soma Zaidi >>

WAZIRI MKUU AADHIMISHA SIKU YA MASHUJAA KWA KUFANYA USAFI COCO BEACH

Waziri mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania mh Kassim Majaliwa ameadhimisha siku ya Mashujaa kwa kufanya usafi katika fukwe za Coco beach ikiwa ni kutekeleza agizo la rais la kutaka siku hii ya kuwakumbuka Mashujaa wetu wananchi waitumie kufanya usafi sehemu mbalimbali.   Waziri mkuu Kassim Majaliwa na mkewe Bi Marry Majaliwa wakifanya usafi pembezoni mwa fukwe za Coco beach Akiambatana na mke wake Bi Marry Majaliwa na kupokelewa na DC wa Kinondoni mh Ally Hapi, waziri mkuu alianza kwa kufyeka nyasi, kuzikusanya na kupeleka katika gari la takataka.…

Soma Zaidi >>

ATHANAS RASMI SINGIDA UNITED

Kuelekea msimu mpya wa ligi kuu soka Tanzania bara maarufu (VPL) klabu ya Singida United imefanya usajili mwengine katika safu ya ushambuliaji kwa kandarasi ya miaka mitatu. Kinda Athanas Mdamu amejiunga na Singida United kama mchezaji huru baada ya kumaliza masomo yake pale Alliance Academy Jijini Mwanza. Akiwa uwanjani Athanas anacheza nafasi ya mshambuliaji wa kati na pembeni.

Soma Zaidi >>

FURSA YA AJIRA TUMAINI UNIVERSITY DAR ES SALAAM COLLEGE (TUDARCO) – HUMAN RESOURCES OFFICER

Tumaini University Dar es Salaam College (TUDARCo) is a centre for quality education, offering a diverse range of academic qualifications. The College offers wide range of undergraduate and Postgraduates programs in social sciences, Education, Business Administration and Laws. Asa  strategy to continue to provide excellent higher education, the College wishes to recruit additional Administrative Staff in the Human Resources Department: Human Resources Officer: 1 posts Qualification, Knowledge and Experience: The candidate must possess a University Degree in Public Administration, Human Resources Management, Personnel Management or Business Administration or possession of…

Soma Zaidi >>