MATAIFA MBALI MBALI KUSHIRIKI RUAHA MARATHON IRINGA JUMAMOSI

WAKATI mji wa Iringa unatarajia kutikiswa jumamosi hii na mashindano ya Ruaha Marathon idadi ya watalii kutoka nchi mbali mbali na wenyeji Iringa wazidi kujiandikisha kushiriki mbio hizo. Afisa habari wa Ruaha Marathon Denis Nyali ameuambia mtandao huu wa Dar Mpya.com kuwa hadi sasa kasi ya watalii toka nchi mbali mbali kufika kujiandikisha ni kubwa sanjari na watanzania. Hivyo alisema katika mashindano hayo ya Ruaha Marathon ambayo yatachochea uchangiaji wa upanuzi wa kituo cha afya Ngome kilichopo kata ya Kihesa bado yataungana na jitihada za serikali ya awamu ya tano…

Soma Zaidi >>

TAARIFA KWA UMMA KUHUSU AJIRA YA WALIMU WA SHULE ZA MSINGI NA SEKONDARI JULAI, 2018 

Ofisi ya Rais -TAMISEMI inapenda kuutarifu Umma kuwa, jumla ya Walimu 4,840 wamepangiwa vituo vya kazi kwenye Shule mbalimbali za Msingi na baadhi kwenye Shule za Sekondari nchini. Walimu hao waliopangiwa vituo vya kazi wanatakiwa kuripoti katika Ofisi za Wakurugenzi wa Halmashauri zilipo shule walizopangiwa na baadaye kuripoti kwenye Shule walizopangiwa. Walimu wote wanatakiwa kuripoti kwenye vituo vyao vya kazi kuanzia tarehe 23 Julai, 2018 hadi tarehe 7 Agosti, 2018 wakiwa na mahitaji yafuatayo: (i) Vyeti halisi vya taaluma vya Kidato cha Nne na/au Kidato cha Sita; (ii) Vyeti halisi…

Soma Zaidi >>

WAIRAQ WAAHIDI KUENDELEA NA MAANDAMANO KUPINGA HALI NGUMU YA MAISHA

Na Tatu Tambile Wairaq wameahidi kuendelea kufanya maandamano katika mji wa Baghdad na mikoa mingine kadhaa kati na kusini wakipinga hali ngumu ya maisha inayowakabili. Waandamaji hao wanadai kuwa na changamoto ya  ukosefu wa ajira inayowapelekea kuwa na hali tete ya maisha. Aidha pia ukosefu wa huduma za kimsingi za jamii, kama vile umeme na maji ya kunywa, ni miongoni mwa madai yao makubwa. Waandamaji hao wameahidi kuendelea na maandamano hayo hadi serikali ya Iraq itakaposikiliza matakwa yao.

Soma Zaidi >>

WAVUVI GHANA WAKATAA ZUIO LA SERIKALI

Na Tatu Tambile Jumuiya ya wavuvi nchini Ghana wamepinga vikali zuio la serikali kufanya shughuli za uvuvi ndani ya mwezi mmoja. Zuio hilo limetolewa na  Waziri wa uvuvi, Elizabeth Afoley Quaye ambaye amesema kuwa katazo hilo linaanza Agost 7 na litahusisha uvuvi wote wa bahari ya Atlantic na nchi kavu hususani uvuvi wa samaki aina ya tuna. Amesema lengo ni kupata manufaa ya kuongezeka kwa idadi ya samaki. Nae kiongozi mkuu wa chama cha wavuvi kilichopo kwenye makao makuu nchini humo jijini Accra, amelalamika kwa kutoshirikishwa na maamuzi hayo na…

Soma Zaidi >>

WAGOMBEA UDIWANI VYAMA VYA UPINZANI KIMARA WAKOSA SIFA ZA KUGOMBEA

Na Tatu Tambile Msimamizi wa uchaguzi wa Manispaa Ubungo ndugu John Kayombo amewaondoa wagombea wa vyama vya Cuf, Chadema na Act Wazalendo kwenye uchaguzi wa kata ya Kimara kwa kukosa sifa za kugombea. Akizungumza na waandishi wa habari msimamizi huyo alisema, wagombea hao wameondolewa baada ya kuwekewa pingamizi na mgombea wa chama cha Mapinduzi ndugu Paschal Manota. Aidha Msimamizi huyo wa uchaguzi ametaja sababu za kuondolewa kwa wagombea hao ni pamoja na kushindwa kuwasilisha fomu za viapo vyao mbele ya tume ya uchaguzi. Kutokana na kushindwa kutekeleza taratibu za tume…

Soma Zaidi >>

UTAJIRI MKUBWA KILOLO UPO UNAKUJA KUPITIA ZAO LA PARACHICHI -DC ASIA ABDALAH

WAKATI serikali ya  awamu ya  tano  chini ya  Rais Dkt  John Magufuli  ikiendelea  kuibua  viwanda  ili  kuwezesha  Taifa  kufikia  uchumi  wa kata  ,mkuu  wa  wilaya ya  Kilolo mkoani Iringa Asia Abdalah amesema  wananchi wa  Kilolo  wategemee kuwa mamilionea kupitia  zao la kilimo  cha Parachichi . Akizungumza na mtandao  huu wa  Darmpya  leo mkuu  huyo wa  wilaya  alisema  kuwa  moja ya mkakati wa wilaya ya  Kilolo ni kuona wananchi  wake  wanajikwamua  kiuchumi na wanakuwa  wanufaika  wakubwa wa uchumi  iwapo kila mmoja  atajikita katika kilimo cha Parachichi . Kwani  alisema  uchumi wa …

Soma Zaidi >>

MCHUNGAJI TITO MWINGINE WA ZIMBABWE AKAMATWA NA POLISI KWA KUUZA TIKETI ZA KWENDA MBINGUNI

HARARE. Hakika Dunia ina mambo tena sana na binadamu katika enzi hizi hutumia kila mbinu kuhakikisha anavuna kutoka kwa mwenzake, huko nchini Zimbabwe Mchungaji mmoja amekamatwa na jeshi la polisi alipokuwa akiwauzia tiketi waumini wake akisema zitawawezesha kuingia mbinguni. Pasta huyo aliyejulikana kwa jina la Tito Wats, pamoja na mke wake wamekuwa wakiwauzia kondoo wake tiketi za kwenda mbinguni kwa Dola 99.4 sawa na zaidi ya Tshs Laki Mbili na Elfu Ishirini. Kulingana na mchungaji huyo, Yesu alimjia binafsi na kumshauri aanze kuuza tiketi hizo. Mbinu iliyotumiwa na mchungaji mmoja wa Zimbabwe…

Soma Zaidi >>

MAGUFULI AITAKA AFRIKA KUUNGANA PAMOJA KATIKA MAPAMBANO DHIDI YA UMASKINI

DAR ES SALAAM. Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. John Pombe Magufuli, amesema huu ni wakati kwa nchi za Afrika, kuungana pamoja katika mapambano dhidi ya umaskini kwa kuandaa misingi bora ya kiuchumi Rais Magufuli amesema hayo leo Juali 17 wakati akifungua mkutano wa kidunia wa vyama vya siasa uliovikutanisha vyama zaidi ya vyama 40 kutoka bara la Afrika na Chama cha Kikomunisti cha China (CPC). Miongoni mwa vyama hivyo, saba (07) vilishiriki katika harakati za ukombozi kusini mwa Afrika ikiwamo CCM.…

Soma Zaidi >>

WATU 40 WAPOTEZA MAISHA KWENYE MAFURIKO NIGERIA

Na Tatu Tambile Taarifa kutoka nchini Nigeria zinasema kuwa takribani watu 40 wamepoteza maisha kufuatia mafuriko yaliyosababishwa ba mvua nyingi katika jimbo la Kaskazini mwa nchi hiyo. Tukio hilo linaripotiwa kutokea usiku wa  Jumapili Julai 15, 2018 ambapo mvua kubwa ilinyesha mfululizo kwa takribani masaa manne. Kwa mujibu wa taarifa kutoka kwa maafisa wa hali ya hewa nchini humo wamesema mafuriko hayo yametokea katika eneo lililo mpakani na Niger, ambapo tayari miili 22 imezikwa na mingine 18 imerejeshwa nchini Niger, ambako miili hiyo ilisombwa na maji. Mafuriko hayo pia yalisababisha…

Soma Zaidi >>

CCM WATUMISHI WA UMMA WATAPATA TABU SANA CHADEMA IKIFA -MCHUNGAJI MSIGWA

Mwenyekiti wa chama cha Demokrasia na maendeleo (CHADEMA) kanda ya Nyasa mchungaji Peter Msigwa amesema watumishi wa umma  Manispaa ya Iringa na CCM watapata tabu sana Chadema ikifa. Mchungaji Msigwa ambae ni mbunge wa jimbo la Iringa mjini ametoa kauli hiyo Leo wakati akizungumza na wanahabari juu ya kasoro mbali mbali za uchaguzi mdogo Tunduma,Wanging’ombe mkoani Njombe na Iringa mjini. Alisema Chadema haipotayari kuiachia Halmashauri ya Manispaa na kuwa katika kata hizo tatu watashiriki uchaguzi na hawatasusa japo wanaamini ushindi Upo Chadema na kama watashindwa bado CCM haitachukua halmashauri hiyo.…

Soma Zaidi >>