KAHAMA YAZIDI KUKALIWA KOONI, WAZIRI MKUU NAE ATOA NENO

Yakiwa yamepita masaa machache tu toka taarifa kutoka Ikulu itangaze kufutwa kazi kwa aliyekuwa Mkuu wa Wilaya hiyo, ndugu Fadhili Nkurlu, Waziri Mkuu Kassim Majaliwa nae katoa neno kwa watumishi wilayani humo.  Waziri mkuu Kassim Majaliwa amekemea mahusiano mabaya baina ya watumishi wa wilaya ya Kahama na kusema wanapaswa kubadilika mara moja.  Ametoa onyo hilo wakati akizungumza na watumishi na viongozi wa Halmashauri za Wilaya za Ushetu, Msalala na Kahama Mji, wilayani Kahama mkoani Shinyanga.  “Hali ya mahusiano hapa Kahama ni mbaya kuliko Kishapu na Shinyanga. Mnachapa kazi vizuri lakini…

Soma Zaidi >>

SASA ZAMU YA WAKUU WA WILAYA, RAIS MAGUFULI AMTUMBUA DC KAHAMA

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli, ametangaza kumfuta kazi aliyekuwa Mkuu wa Wilaya ya Kahama mkoani Shinyanga, ndugu Fadhili Nkurlu. Kwa mujibu wa taarifa kutoka Ikulu zinasema kuwa, Rais Magufuli amefikia uamuzi huo hii leo Julai 15, 2018. Kufuatia hatua hiyo, Rais Magufuli amemteua Anamringi Macha kuwa Mkuu wa Wilaya ya Kahama. Mkuu wa Wilaya, Anamringi Macha ametakiwa kuripoti katika kituo chake cha kazi mara moja. Hata hivyo taarifa hiyo haijaeleza sababu za Rais Magufuli kufikia uamuzi wake wa kumtumbua ndugu Fadhili Nkurlu.

Soma Zaidi >>

WORLD CUP-2018 FINAL:NANI ZAIDI BAINA YA UFARANSA ALIYESAHAU KIKOMBE HIKI KWA MIAKA 20 DHIDI CROATIA

MOSCOW. Leo ikiwa ni siku ya fainali za kombe la dunia kwa mwaka 2018, michuano ambayo ilikuwa ikichezwa nchini Urusi, ni watu wachache walitarajia wakati tamasha hilo kubwa la kandanda duniani lilipoanza wiki nne zilizopita. Croatia inachuana na Ufaransa mjini Moscow ikijaribu kunyakua taji la kombe la dunia kwa mara ya kwanza, huku kikosi cha kocha Didier Deschamps wa Ufaransa kinalenga kupata taji lake la pili, tangu 1998. Timu ya taifa ya Croatia imeleta furaha katika taifa hilo la Balkan ambalo lina Wakazi Milioni 04 tu kwa kwenda kinyume na…

Soma Zaidi >>

WAZIRI ATOA WIKI 6 KWA MKANDARASI KUMALIZA KUWEKA LAMI BARABARA YA NYAKANAZI – KABINGO

Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Isaac Kamwelwe ameipa wiki sita kampuni inayojiusisha na ujenzi wa barabara Nyanza Road Works, kuhakikisha inakamilisha zoezi la kuweka lami barabara ya Nyakanazi – Kibingo. Kamwelwe amesema barabara hiyo inapaswa kuwekwa lami Kilomita 23 kati ya 50 inazozijenga katika barabara hiyo ambayo ujenzi wake umeanza tangu mwaka 2014. Waziri Kamwelwe amesema kuwa endapo mkandarasi huyo atashindwa kukamilisha uwekwaji lami katika kipande hicho, basi atanyang’anywa kazi hiyo na kupewa mkandarasi mwingine. Barabara ya Nyakanazi – Kabingo inapatikana mkoani Kigoma ambapo imekuwa ikitumika kama kiunganishi cha…

Soma Zaidi >>

ASHIKILIWA NA JESHI LA POLISI KWA KUIBA KICHANGA CHA MIEZI 2

Mama mmoja aliyetambulika kwa jina la Bi.Habiba Abubakari, anashikiliwa na jeshi la polisi mkoani Shinyanga kwa tuhuma za kuiba mtoto mchanga wa miezi miwili mkoani Singida. Inadaiwa kuwa mtuhumiwa alimuiba mtoto huyo mkoani Singida na kisha kutoroka naye hadi wilayani Kahama na kujificha. Baada ya kutoweka kwa mwanae, mama mzazi wa mtoto huyo, Bi.Hawa Roggers alitoa taarifa kwa vyombo vya ulinzi na usalama, na ndipo jitihada za kumsaka mtuhumiwa zilipoanza mara moja na kufanikiwa kumpata mtuhumiwa huko mkoani shinyanga. Tayari Bi.Hawa Roggers amekabidhiwa mtoto wake na Kamanda wa Polisi Shinyanga…

Soma Zaidi >>

MATUKIO KUELEKEA UCHAGUZI MDOGO WA MARUDIO AGOSTI 12, GODBLESS LEMA ALALAMA

Zikiwa zimesalia takribani siku 28 kuelekea kufanyika kwa uchaguzi mdogo wa marudio kote nchini, Mbunge wa Arusha Mjini (CHADEMA) Godbless Lema, ameibuka na kulalamikia baadhi ya matukio yasiyokuwa yakiungwana ambayo yamekuwa yakiendelea katika maeneo mbalimbali hapa nchini. Akiandika katika ukurasa wake wa Twitter, Mbunge Lema ameilalamikia CCM na Ofisi ya Msimamizi Msaidizi katika kata ya Terrat, kushiriki katika kufanya vitendo vya hujuma dhidi ya mgombea wa CHADEMA katika kata hiyo ndugu Raymond Laizer. Lema amesema kikundi cha ulinzi CCM ‘green guard’ walishiriki kumpora fomu ndugu Raymond Laizer akiwa kwenye ofisi…

Soma Zaidi >>