CROATIA WAIFATA UFARANSA FAINALI KOME LA DUNIA

Nchini Urusi ,mchezo wa nusu fainali ya pili kati ya timu ya taifa ya Uingereza dhidi ya timu ya taifa ya Croatia umekwisha kwa timu ya taifa ya Croatia kujihakishia ticket ya kucheza fainali ,tarehe 15/07/2018 katka dimba la Luzhnik ndani ya jiji la Moscow. Katika mchezo huo timu ya taifa ya Uingereza ilikuwa ya kwanza kujiandikiwa goli katika kipindi cha kwanza kupitia kwa mlinzi wa klabu ya Tottenham K. Trippier kwa adhabu ndogo  iliyomshinda  mlinda mlango  wa Croatia Danijel Subasic nakukwama nyavuni, kipndi cha pili Croatia walirejea mchezoni baada…

Soma Zaidi >>

ALIYEWATAPELI WATALII DOLA 5000 AKAMATWA

Jeshi la Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam inamshikilia Omwailimu Sosthenes ambaye ni mmiliki wa kampuni ya Utalii ya  Arise Special Sunrise,kwa tuhuma za kuwatapeli watalii wawili Dola za kimalekani 5000. Akizungumza na waandishi wa habari leo jijini Dar es Salaam, Kaimu Kamanda wa Polisi Kanda Maalum, DCP Liberatus Sabas, amesema mtuhumiwa huyo aliwatapeli watalii hao ambaye mmoja anaishi Marekani na mwingine nchini India kwa makubaliano kwamba angewapeleka safari ambazo walizipanga. Amesema baada ya mtuhumiwa huyo kuwatapeli wageni hao aliwatelekeza katika nyumba ya wageni maeneo ya Sinza na walipojaribu…

Soma Zaidi >>

MWANAMKE MMOJA NA MTUHUMIWA WA KUNDI LA KIGAIDI NCHINI UJERUMANI AFUNGWA MAISHA

MUNICH. Nchini Ujerumani Mahakama moja ya mjini Munich imemhukumu kifungo cha maisha, Bibi Beate Zschaepe aliyekuwa mwanachama wa kundi la kigaidi la NSU lililokuwa linalojiita Wanazi mamboleo, ambaye ni mtuhumiwa mkuu katika kesi iliyohusu vuguvugu la chini kwa chini nchini humo. Mahakama ilitoa uamuzi huo leo hii Jumatano ambapo Bibi Zschaepe amepewa hukumu hiyo ya kifungo cha maisha. Mshtakiwa huyo amekutwa na hatia kuhusiana na maujai ya watu 10 wengi wao wakiwa ni wahamiaji wa Kituruki ambao waliuwawa kwa kupigwa risasi kati ya mwaka 2000 na 2007. “Kesi hii ilisababisha…

Soma Zaidi >>

CHELSEA WAIFANYIA MANCHESTER CITY KITU MBAYA

 Baada ya kuzagaa kwa taarifa za kiungo wa klabu ya Napoli Jorginho kujiunga na klabu mabingwa wa ligi kuu nchini Uingereza ,Manchester city . Jana katika mji wa Capri nchini Italia kulikuwa na kikao  kati ya raisi wa klabu ya Napoli Aurelio De Laurentiis  na mmiliki wa klabu ya Chelsea Roman Abrahamovic  wawili hao wamefikina makubalinao ya Chelsea kupata saini  ya Kiungo wa Napoli Jorginho na aliyekuwa mkufunzi wa Klabu hiyo Maurzio Sarri kwa dau la paundi million 65, paundi million 8 kwa kocha Sarri na 57 kwajiri ya kiungo Jorginho.…

Soma Zaidi >>

‘TUMETEKELEZA AHADI KWENYE KATA ZINAZOONGOZWA NA CHAMA CHETU’, ACT WAZALENDO.

Mapema siku ya leo Julai 11, 2018, chama cha ACT Wazalendo kimetoa taarifa ya utekelezaji wa ahadi ilizozitoa katika kata zinazoongozwa na chama hicho, wakati wa ziara maalumu ya kutembelea kata hizo kati ya tarehe 19 Februari hadi tarehe 9 Machi mwaka huu. Akitoa taarifa ya utekelezaji wa ahadi hizo kwenye ofisi za makau makuu ya chama hicho jijini Dar es Salaam, Katibu Bunge na Serikali za Mitaa, ACT Wazalendo, mama Janeth Rithe amesema kuwa mara baada ya kuhitimisha ziara hiyo, chama kilianzisha harambee kwa wanachama na viongozi kwa ujumla…

Soma Zaidi >>

UGANDA POLISI WATUMIA MABOMU KUWATAWANYA WAANDAMANAJI WA KUPINGA KODI YA MITANDAO YA KIJAMII

KAMPALA. Nchini Uganda Jeshi la polisi limetumia mabomu ya machozi leo kuwatawanya mamia ya waandamanaji katika mitaa mbalimbali, ambao walikuwa wanapinga tozo jipya la kodi kwa matumizi ya mitandao ya kijamii. Vyombo vya habari nchini humo vimeripoti kuwa polisi pia walijaribu kumkamata kiongozi wa maandamano hayo Mwimbaji Robert Kyagulanyi, ambaye pia hujulikana kama “Bobi Wine”, Mbunge wa jimbo la Kyaddondo Mashariki kutoka wilaya ya Wakisso Mkoa Kati nchini humo lakini alifanikiwa kukimbia. Kodi hiyo iliyoanza kukatwa mwanzoni mwa mwezi huu, inamlazimu mtumiaji wa mitandao kama Facebook, WhatsApp Twitter na hata…

Soma Zaidi >>

UNILEVER TANZANIA LTD YAKABIDHI ZAWADI KWA WASHINDI WA PROMOSHENI YA ‘ONJA LADHA USHINDE’

Kampuni ya Unilever Tanzania Limited, Siku ya jana  Julai 10, 2018 imekabidhi zawadi kwa washindi wanne kati ya sita walioibuka kidedea katika  promosheni ya Onja Ladha Ushinde. Akikabidhi zawadi hizo Meneja wa Fedha wa Kampuni hiyo, Raymond Antony amewataja washindi hao kuwa ni pamoja na Kenedy Wilfred na Himida ambao kila mmoja amejinyakulia kitita cha shilingi 50,000/=, huku washindi wengine Upendo Frank kutoka Sayansi Kijitonyama na Godfrey Francis kutoka Kisutu wakijishindia Mbuzi kwa kila mmoja. Akieleza sababu ya kuanzishwa kwa promosheni hiyo, Raymond amesema wameamua kurudisha faida ya kile kinachopatikana…

Soma Zaidi >>