RONALDO SAFARI YA KWENDA JUVENTUS IMEIVA.

Baada  ya  majarida mengi ya michezo duniani kuandika juu ya uhamisho wa mshambuliaji hatari wa timu ya taifa ya ureno na klabu ya Real Madrid Christian Ronaldo. Dhahiri safari inaonekana kuiva kwa Ronaldo kuondoka ndani ya klabu ya Real Madrid na  kujiunga kunako klabu mabingwa wa nchini Italia Juventus, taarifa ya juzi ilionyesha jinsi uongozi wa klabu ya Madrid kuweka wazi uhamisho wa Ronaldo ilaa ulimuomba Ronaldo atumie muda huo wa siku kadhaa kabla ajajiunga na Juventus kuwambia mashabiki wa klabu ya Real Madrid yakwamba yeye ndio anataka kuondoka wala…

Soma Zaidi >>

UBUNGO KUUPOKEA MWENGE WA UHURU KWA KISHINDO

Wilaya ya Ubungo iliyopo mkoani Dar es Salaam imesema ipo tayari kuupokea Mwenge wa Uhuru kwa kishindo kikubwa, na kuwa tayari wananchi wamejiandaa vya kutosha kupamba mapokezi ya mwenge huo. Hayo yamesemwa asubuhi ya leo Julai 9, 2018 na Mkuu wa Wilaya hiyo Mhe. Kisare Makori alipokuwa akizungumza na waandishi wa habari ofisini kwake,  Kibamba jijini Dar es Salaam. Mhe. Makori amesema kuwa wilaya yake itaupokea mwenge huo siku ya kesho tarehe 10 Julai, 2018 ukitokea wilaya ya Kinondoni, ambapo baada ya kutoka wilayani Ubungo mwenge huo utaelekea katika wilaya…

Soma Zaidi >>

WAZIRI ALIYESIMAMIA MCHAKATO WA UINGEREZA KUJIONDOA EU (Brexit) NA NAIBU WAKE WAJIUZULU

  Waziri wa masuala ya Uingereza kujitenga na Umoja wa Ulaya maarufu kama “Brexit”, ambaye pia ni Mjumbe mkuu wa Uingereza katika mazungumzo ya nchi hiyo kujiondoa katika Umoja wa Ulaya, David Davis, amejiuzulu. Usiku wa kuamkia leo Davis alijiuzulu pamoja na Naibu wake, kwa sababu alitofautiana na msimamo wa serikali yake ambao baraza la mawaziri lilikubaliana nao siku chache zilizopita. Kwenye barua yake ya kujiuzulu kwa Waziri Mkuu Theresa May, Davis amesema sera na mbinu zilizoko kwa sasa, zinaifanya Uingereza kuwa na nafasi ndogo au haitajitenga na umoja wa…

Soma Zaidi >>

WAZIRI MKUU WA ETHIOPIA AREJESHA MAHUSIANO YA KIDIPLOMASIA & KIBIASHARA NA ERITREA

  Waziri Mkuu wa Ethiopia Abiy Ahmed, wiki hii aliwasili nchini Eritrea katika ziara yake ikiwa ni baada ya mwezi mmoja kuyatambua kikamilifu makubaliano yaliyomaliza vita vya mpaka baina ya nchi hizo ndugu, ambavyo vilidumu kwa miaka miwili. Kiongozi wa muda mrefu wa Eritrea Isaias Afwerki alimkaribisha Abiy katika uwanja wa ndege wa Asmara kabla ya kuelekea katika Ikulu kwa ajili ya mazungumzo yaliyodumu siku nzima. Kuwasili kwake kumeonyeshwa moja kwa moja na televisheni ya taifa ya Eritrea, na kundi kubwa la watu lilionekana limevalia fulana zenye picha za viongozi…

Soma Zaidi >>

MANJI “YANGA NIPENI MUDA KIDOGO.

Kwenye mkutano ulifanyika katika ukumbi wa Bwalo la polisi Ostarbay  jijini Dar es salaam,aliyekuwa mwenyekiti wa Yanga Yusufu Manji alituma barua kwa viongozi wa Yanga juu ya kujiuzulu kwake kama mwenyekiti wa Yanga. Lakini ombi la Manji kujiuzulu lilipingwa vikali na viongozi wa matawi wa Yanga ,na wengi wao wakidai licha ya matatizo ambayo Manji amepitia ila bado wanamtambua Manji kama mwenyekiti wa klabu hiyo. Jana akiongea na vyombo vya habari jijini Dar es salaam ,Makamu mwenyekiti wa klabu ya Yanga ,ndugu Clement Sanga,amesema “Manji amekubali kurudi na kuendelea kuwa…

Soma Zaidi >>

RIEK MACHAR MBIONI KUREJESHEWA WADHIFA WAKE

Kiongozi wa kisiasa maarufu nchini Sudan Kusini na aliyekuwa Makamu wa rais wa zamani wa nchi hiyo, Riek Machar, atarejeshwa katika wadhifa wake kama sehemu ya makubaliano ya amani ya kuvifikisha mwisho vita vya karibu miaka mitano ambavyo vimewaua maelfu ya watu na kuliharibu kabisa taifa hilo changa barani Afrika. Makubaliano hayo yaliafikiwa katika mazungumzo ya mjini Entebbe, na yalisimamiwa na Rais Yoweri Museveni wa Uganda na kuhudhuriwa na Rais wa Sudan Kusini Salva Kiir, Rais wa Sudan Omar al-Bashir na Machar. Taarifa ya ofisi ya rais ya Sudan Kusini…

Soma Zaidi >>

MAUZO DSE YAPOROMOKA

Mauzo ya Hisa katika Soko la Hisa la Dar es Salaam (DSE) yameshuka kutoka Sh bilioni 1.11 wiki iliyopita hadi Sh milioni 676.26 wiki hii. Akizungumza na waandishi wa habari leo jijini Dar es Salaam, Mkurugenzi wa Biashara na Masoko, Emanuel Nyalali, amesema mauzo hayo yametokana na kuuzwa kwa mihamala 166. “Wakati huo thamani ya Soko la Hisa imeongezeka hadi kufikia Sh trilioni 22.18 kutoka Sh 21.99 wiki iliyopita,” amesema Nyalali. Aidha amesema katika kipindi hicho, hatifungani za serikali na makampuni zenye thamani ya Sh bilioni 1.96 ziliuzwa kwenye mihamala…

Soma Zaidi >>