MTANDAO WA WANAFUNZI (TSNP) WATOA TAMKO TIMUA TIMUA YA WANACHUO BUGANDO

Mtandao wa Wanafunzi Tanzania (TSNP) umetoa tamko kuhusu suala la kufukuzwa kwa wanafunzi na viongozi wa wanafunzi katika chuo cha Bugando. Kupitia taarifa yake kwa vyombo vya habari hii leo, TSNP imesema imepokea taarifa ya wanafunzi 10 wa Chuo cha Catholic University of Health and Allied Science (CUHAS-BUGANDO) kufukuzwa na kusimamishwa masomo, ambapo imedai kuwa katika idadi hiyo ya wanafunzi kumi, wanafunzi wawili ndio waliofukuzwa . Imewataja waliofukuzwa kuwa ni aliyekuwa Rais wa Serikali ya Wanafunzi, ndugu Timon Stephen, na aliyekuwa Spika wa Bunge la Wanafunzi 2016/17, ndugu Godfrey Lameck.…

Soma Zaidi >>

NI GOR MAHEA TENA, BINGWA WA SPORT PESA.

Fainali za michuano ya ligi ya Sport pesa zimekoma leo June 10, 2018 katika uwanja wa Afraham Jijini Nakuru nchini Kenya, huku timu ya Gor mahea ikiibuka bingwa kwa mara nyingne tena  baada ya kuifunga Timu ya Simba kutokea Tanzania magoli 2:0. Mchezo huo uliokuwa wa pili kuchezwa jumapili ya leo katika fainali hizo huku  mchezo wa kwanza wa kumtafuta mshindi wa tatu uliwakutanisha Singida united ya Tanzania dhidi ya Kaka mega boys ya Kenya na kumalizika kwa kufungana 1:1. Gor mahea walionyesha hamasa ya kutafuta goli la mapema katika…

Soma Zaidi >>

DIWANI WA CCM APOTEZA MAISHA KWA AJALI ASUBUHI YA LEO.

Diwani wa CCM katika kata ya Tindabuligi wilayani Meatu mkoani Simiyu, ndugu Seleman Mahega amepoteza maisha akiwa katika Hospitali ya Mwandoya alipokuwa akipatiwa huduma ya kwanza mara baada ya kuapata ajali asubuhi ya leo. Diwani huyo ni mmoja wa wale waliokuwa kwenye msafara wa mwenyekiti wa Uvccm Taifa Kheri James, uliopata ajali asubuhi ya leo mara baada ya magari katika msafara huo kugongana baada ya moja ya gari kwenye msafara kufunga breki ya ghafla iliyosababisha kutokea vumbi lilipelekea madereva katika magari ya nyuma yake kushindwa kuona vizuri. Taarifa za msiba…

Soma Zaidi >>

G7 WAKUBALIANA KUCHANGIA BILIONI 3 KWAAJILI YA ELIMU KWA WASICHANA.

Mkutano wa nchi saba zenye nguvu ya viwanda duniani, G7 umekubaliana kuchangia jumla ya shilingi bilioni 3 kwaajili ya kuboresha elimu kwa upande wa wanafunzi wa kike. Hayo yamebainishwa hapo jana wakati wa zoezi la kufunga mkutano wa nchi hizo uliofanyika huko Quebec nchini Canada. Mwenyeji wa mkutano huo nchi ya Canada imesema imesema kuwa  itachangia kiasi cha pauni bilioni 2.9 ikisaidiwa na nchi washirika wa G7 kwa ajili ya mpango huo wa kusaidia elimu ya wasichana na wanawake walio masikini. Fedha hizo zitasaidia kuhakikisha kuwa mpango wa wasichana na…

Soma Zaidi >>

UFAHAMU MPIRA UTAKAOTUMIKA KWENYE FAINALI ZA KOMBE LA DUNIA NCHINI URUSI.

Na Azizi – Mtambo 15. Zikiwa zimebakia siku kadhaa kuelekea kwenye michuano ya kombe la dunia itakayofanyika nchini Urusi, leo tuchambue mpira utakaotumika kwenye mashindano hayo. TELESTAR 18. Mpira huo ndo utakaotumika kuelekea kwenye fainali za kombe la dunia. Mpira huo umetengenezwa na kampuni ya Ujerumani,  ambayo inatengeneza vifaa vya michezo vya Adidas. Mpira huo ulitengenezwa mwaka 1970, unaitwa Telestar ulianza kutumika katika fainali iliyofanyika nchini Mexico. Mpira huo unauzwa Dolla za Kimarekani 100 ambazo ni sawa na shilingi 2,2700 za Kitanzania. Mpira huo umetengenezwa katika kiwango cha hali ya…

Soma Zaidi >>