MWANA MASUMBWI FLORD MAYWEATHER  ATAJWA KUWA MCHEZAJI TAJIRI ZAIDI DUNIANI

Mchezaji wa masumbwi wa Marekani Floyd Mayweather ametetea taji lake katika orodha ya Forbes ya wanamichezo wanaopata mapato ya juu zaidi duniani. Alijipatia kipato cha $275m (£205m) katika mechi yake ya masumbwi mwezi Agosti dhidi ya nyota wa UFC star Conor McGregor, ambaye yuko nambari nne katika orodha ya jarida hilo la biashara nchini Marekani. Cristiano Ronaldo ambaye alikuwa akiorodheshwa wa kwanza katika kipindi cha miaka 2 iliopita, sasa ni wa tatu huku Lionel Messi akichukua wadhifa wa nafasi ya pili kwa tofauti ndogo. La kushangaza ni kwamba hakuna wanawake…

Soma Zaidi >>

BREAKING NEWS :BASI LAIGONGA TRENI NA KUUWA WATU 7 NA MAJERUHI 27 MKOANI KIGOMA

Na Joel Silver Watu 7 wamefariki dunia na wengine 27 wamejeruhiwa vibaya, baada ya basi la Kampuni ya Hamida kugonga treni ya mizigo mkoani Kigoma. Akithibitisha kutokea kwa ajali hiyo Kamanda wa polisi mkoani Kigoma Martin Otieno, amesema kwamba ajali hiyo imetokea majira ya saa 12:15 asubuhi ya leo katika eneo la Gungu, baada ya basi hilo ambalo linafanya safari zake kutoka Mkoani Kigoma kwenda Tabora, kugonga treni ya mizigo iliyokuwa ikipita kwenye njia yake, licha ya dereva wa treni kupiga honi kumpa tahadhari dereva wa basi. Dereva wa basi…

Soma Zaidi >>

NYUMBA YATEKETEA KWA MOTO JIJINI DODOMA HUKU CHANZO KIKIDAIWA NI JIKO LA GESI

Joel Silver Moto mkubwa unaosemekana umesababishwa na kulipuka kwa jiko la nishati ya gesi umeteketeza nyumba moja yenye vyumba sita iliyopo katika mtaa wa hazina x jijini Dodoma na kuharibu mali za baadhi ya wapangaji waliokuwa wakiishi ndani ya nyumba hiyo Wakizungumza na waandishi wa habari baadhi ya wapangaji wa nyumba hiyo Maimuna Hussein na Nickson Steven wamesema moto huo umetokea asubuhi na kuteketeza baadhi ya mali zao. Kwa upande wake Mkuu wa kikosi cha zimamoto na uokoji mkoa wa Dodoma, kamishna msaidizi Regina Kaombwe, amesema baada ya kupata taarifa…

Soma Zaidi >>