YANGA WAIPA SIMBA UBINGWA WA LIGI KUU BARA.

Timu ya soka ya Yanga ni kama imewapa ubingwa wa Ligi Kuu Bara, maarufu kama VPL, watani wao wa jadi, Simba, kufuatia kukubali kipigo cha 2-0 kutoka kwa wajela jela Tanzania Prisons. Katika mchezo wa ligi kuu uliochezwa jioni ya leo katika dimba la Sokoine jijini Mbeya, Yanga imekubali kipigo hicho kupitia kwa magoli ya Eliuter Mpepo aliyefunga kwa njia ya penati katika dakika ya 58, na Salum Bosco aliyefunga katika dakika ya 85. Yanga wanavuliwa rasmi ubingwa wa Ligi Kuu Tanzania Bara, na kuelekea mtaa wa Msimbazi, kutokana na…

Soma Zaidi >>

JESHI LA MAGEREZA LATOLEA UFAFANUZI UTATA WA MBUNGE ‘SUGU’ KUACHIWA HURU.

Jeshi la Magereza limetolea ufafanuzi utata kuhusu kuachiwa kwa Mbunge wa Mbeya Mjini, Joseph Mbilinyi na mwenzake, kufuatia mjadala ulioibuka kwenye mitandao ya kijamii ukidai kuwa kuachiliwa kwao ni kwa kiholela, yaani hakuna sababu maalumu zilizotolewa. Ufafanuzi huo umetolewa mchana wa leo na Kamishina Jenerali wa Magereza, Dkt. Juma A. Malewa, ambaye ametaja sababu ya kuachiwa kwao kuwa kunatokana na msamaha na Rais Magufuli, alioutoa wakati wa Maadhimisho ya Sherehe za Muungano Aprili 26 mwaka huu. Kamishina Malewa kupitia taarifa yake anasema kuwa mheshimiwa Sugu ni miongoni mwa wafungwa 3,319…

Soma Zaidi >>

SERIKALI KUBORESHA MIUNDOMBINU SOKO LA MAGOMENI, DAR ES SALAAM.

Serikali kupitia Wizara ya Nchi, Ofisi ya Rais TAMISEMI, imetangaza kuboresha miundombinu katika soko la Magomeni lililopo katika Manispaa ya Kinondoni, jijini Dar es Salaam. Ahadi hiyo imetolewa siku ya leo Mei 10, 2018, na waziri wa wizara hiyo, Mhe. Suleiman Jafo alipofanya ziara kwenye soko hilo kukagua hali ya miundombinu, ikiwa ni pamoja na uchakavu wa vizimba, ambapo alipata fursa pia ya kufanya mazungumzo na wafanyabiashara wa soko hilo. Jafo amesema nia ya serikali ni kuona masoko yote yapo katika hali nzuri inayowawezesha wafanyabiashara kufanya biashara zao kwa urahisi…

Soma Zaidi >>

NI MWENDO WA MAJANGA TU KWA KANYE WEST.

Huku kukiwa na fukunyunyu ya kwamba penzi lake na mkewe liko katika chungu cha moto likifukuta, Kanye anazidi kuandamwa na mikosi. Hii nikutokana na mfululizo wa matukio ya kupingwa na kwanza kukosa support kutoka kwa watu mbalimbali hasa kipindi hiki akijiaandaa kuachia album zake mbili. Matokeo ya kuunga mkono suala la utumwa na kumuunga mkono bwana Trump inaonekana mambo mengi yataenda kombo kwa rapa Kanye West. Jamaa huyo ambaye yupo mawindoni akipika album mbili ameingia kwenye mzozo mkubwa na watu weusi, wengi raia wa marekani huku pia wanaharakati wakipinga kauli…

Soma Zaidi >>

WOLPER AKINUKISHA TENA.

Ilianza kama masihara kisa Wolper kucoment kwenye post ya Harmonize, Sarah akamind na kumtaka Wolper aache kumfuatilia bebe wake kwa lolote like akimtaka akae mbali kabisa. Mwarabu fighter bodyguard wa Diamond akaingia kwenye stori ambapo post moja ikatoka kumuonyesha yeye na Sarah demu wa Harmonize wakipeana tabasamu matata, ikasemwa Sarah anachepuka na mwarabu fighter. Kwenye interview flani hivi Wolper aliulizwa swali la kizushi kuhusu fukunyunyu za Sarah na Monde boy kutemana, Gambe alionekana kujibu shiti flani hivi ambayo ilimkwaza Harmonize. Kupitia ukurasa wake wa Insta mkali wa kibao cha kwangaru…

Soma Zaidi >>

MASKINI DOGO JANJA!

Ni kama miezi miwili hivi mwanadada mkali kwa kiwanda cha Filamu Tz na pia mjasiriamali Irene Uwoya alichukua hatua kubwa zaidi baada ya kuchora tatoo yenye jina la mumewe kipenzi Abdulaziz Chance “Dogo Janja”. Yap stori zikavuja zaidi kwamba Janjaro pia alitaka kumlipa mkewe, lakini Uwoya alimuonya asichore kwa kukurupuka tu bali aamue kwa dhati, hivyo zoezi likashindikana. Jana ghafla kupitia ukurasa wake wa Insta Dogo Janja aliposti picha akiwa kiwandani kuchora tatoo, pamoja na kwamba muda huo hakikuwa kikionekana chochote, caption ya post hiyo ilikuwa na maneno machache. Kisha…

Soma Zaidi >>

ZITTO KABWE AGOMA KUMPA POLE SUGU BAADA YA KUTOKA GEREZANI

Mbunge wa Kigoma Mjini,  Zitto Kabwe amegoma kumpa pole Mbunge wa Mbeya Mjini , Joseph Mbilinyi ‘Sugu’ pamoja na mwenzie Emmanuel Masonga baada ya kutoka gerezani kwa madai kuwa  viongozi wote wa upinzani kwa sasa ni wafungwa watarajiwa. Zitto Kabwe ameandika katika ukurasa wake wa mtandao wa Twitter kwamba amefurahi kuona wako huru huku akiamini kuwa  kukaa kwao gerezani kumewaongezea ari ya kupigania Demokrasia nchini. “Nafurahi kuwa Mbunge Mbeya Mjini Ndg. Joseph Mbilinyi (Sugu) na mdogo wangu Emmanuel Masonga wametoka Gerezani! siwapi pole, maana katika nyakati za Udikteta wapinzani wote ni wafungwa…

Soma Zaidi >>

SERIKALI YAONGEZA IDADI YA WANAFUNZI WATAKAOPATA MIKOPO

Idadi ya wanafunzi  watakaonufaika na mikopo kutoka Bodi ya Mikopo ya Wanafunzi wa Elimu ya Juu- HESLB imeongezeka kutoka 33,000 hadi 40,000 kwa mwaka wa masomo wa 2018/19. Akizungumza na wanahabari leo jijini Dar es Salaam Mkurugenzi Mtendaji wa HESLB, Abdulrazaq Badru amesema bodi hiyo imeongeza idadi ya zaidi ya wanafunzi 7,000 ukilinganisha na 33,000 waliopata mwaka jana. Badru amesema zimetengwa jumla ya Sh. 437 bilioni kwa ajili ya kutoa mikopo hiyo, ambapo pia HESLB imeongeza wigo wa kutoa mikopo kwa wanafunzi wa stashahada. Amesema hapo awali mikopo ilikuwa inatolewa…

Soma Zaidi >>

SERIKALI YACHUKUA TAHADHARI DHIDI YA UGONJWA WA EBOLA

Serikali imeagiza waganga wakuu katika mikoa yote nchini hasa iliyoko mipakani kuchukua tahadhari dhidi ya mlipuko wa ugonjwa wa ebola. Agizo hilo limetolewa leo na Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Ummy Mwalimu wakati akizungumza na wanahabari ofisini kwake jijini Dodoma. Waziri Ummy amesema waganga wakuu katika mikoa ya mipakani wanatakiwa kuwa na tahadhari kwani mikoa yao inazungukwa nan chi nyingi na hivyo ni rahisi kuwepo kwa muingiliano. Aidha, Waziri Ummy amesema hakuna mtanzania aliyegunduliwa kuwa na viashiria vya ugonjwa huo ambao upo katika nchi ya…

Soma Zaidi >>