TANZIA: MSANII JEBBY AFARIKI DUNIA.

Tasnia ya muziki hapa nchini imepata pigo jingine mara baada ya kumpoteza msanii wa muziki wa Bongo Fleva, Jebby, ambaye amefariki dunia siku ya leo April 22, 2018, huko mjini Dodoma alikokuwa akipatiwa matibabu. Chanzo cha kifo chake kinatajwa kuwa ni ugonjwa wa bandama, ambao kwa maelezo ya ndugu zake, umekuwa ukimsumbua kwa siku nyingi. Marafiki zake wa karibu akiwemo msanii Afande Selle, pia amethibitisha kutokea kwa kifo cha msanii Jebby, ambaye amewahi kutamba na kibao chake cha ‘Swahiba’ambacho walishirikiana na Afande Selle.

Soma Zaidi >>

YANGA KAMA SIMBA, MBEYA.

Timu ya Soka ya Yanga imelazimishwa sare ya bao 1-1, na timu ya Mbeya City, katika mchezo wa ligi kuu uliochezwa jioni hii, katika dimba la Sokoine, jijini Mbeya. Yanga ndio walikuwa wa kwanza kujipatia bao katika dakika ya 58 ya mchezo kupitia kwa mchezaji wake aitwaye Raphael Daud, bao ambalo Yanga walionekana kulizika nalo, na kupunguza mashambulizi kwenye lango la Mbeya City. Wabishi wa Mbeya City wamefanikiwa kusawazisha bao hilo kupitia kwa mshambuliaji wake Idd Suleiman, katika dakika ya 91, ikiwa ni kwenye muda wa dakika 6 za nyongeza…

Soma Zaidi >>

DIAMOND PLATNUMZ ASABABISHA KIZAA ZAA, SHUGHULI YA KUAGA MWILI WA MAREHEMU MASOGANGE.

Dar es Salaam. Msanii wa Bongo Fleva na kiongozi wa kundi la Wasafi ‘WCB’, Naseeb Abdul, maarufu kama Diamond Platnumz, amesababisha kizaa zaa kwenye viwanja vya Leaders, katika shughuli za kuuaga mwili wa marehemu Agnes Gerald Waya, maarufu kwa jina la Agnes Masogange. Diamond amesababisha kizaa zaa hicho mara baada ya mwenyekiti wa kamati ya mazishi, Steven Nyerere, kumkaribisha kwaajili ya kutoa salamu zake za pole kwa wafiwa na watu wote walikuwa kwenye viwanja hivyo. Mara baada ya kusikia Diamond anakuja kuzungumza, waandishi wa habari waliokuwa kwenye viwanja hivyo, walianza…

Soma Zaidi >>

POLEPOLE AWACHARUKIA WANAOMKOSOA.

Katibu wa Itikadi na Uenezi CCM, Humphrey Polepole, amewacharukia wakosoaji wake, wanaodai kuwa amepoteza mwelekeo kwa kitendo chake cha kuitetea serikali, mara baada ya ripoti ya CAG kuonesha kuwa serikali imepata hati chafu, kwa kutoonekana matumizi ya kiasi cha pesa Trioni 1.5, kwenye ripoti ya CAG ya mwaka 2016/17, iliyowasilishwa mapema mwezi huu wa April. Kupitia katika ukurasa wake wa Twitter, Polepole amewataka wale wote wanaoituhumu serikali ya awamu ya tano chini ya Rais Maguguli, kuwa imelisababishia taifa hasara, kuthibitisha madai hayo, na kuacha kupiga porojo kwenye mitandao ya kijamii.…

Soma Zaidi >>

SIMBA ILICHEZA KICHOVU SANA-MATOLA

Kufuatia mtanange wa jana katika ligi kumalizika kwa sare ya bao 1-1 dhidi ya Simba, Kocha Suleiman Matola ashangazwa na kiwango cha wapinzani wake. Matola alieleza kushangazwa na Simba kucheza chini ya kiwango kitu ambacho ni tofauti na namna timu hiyo ilivyoanza harakati za kuwania ubingwa mwanzoni mwa msimu wa ligi. Kocha huyo alisema Simba ilicheza tofauti na michezo mingine na kujikuta akijiuliza haswa tatizo lilikuwa ni nini. Akizungumza bada ya mchezo kumalizika, Matola alisema vilevile timu yake ilicheza vizuri zaidi ya Simba na ilipata nafasi nyingi ingawa ilishindwa kuzitumia…

Soma Zaidi >>

IKUFIKIE TAARIFA HII MUHIMU KUTOKA MAMLAKA YA HALI YA HEWA.

Mamlaka ya Hali ya Hewa Tanzania (TMA) imesema hali ya mvua katika maeneo mengi ya nchi itapungua kuanzia usiku wa leo Aprili 21, 2018. Taarifa ya TMA iliyotolewa jana imesema maeneo mengi ya nchi yanatarajiwa kuwa na hali ya mawingu kiasi, mvua nyepesi katika maeneo machache na vipindi vya jua. Pia, TMA imesema maeneo mengine ya mikoa yatakuwa na hali ya mawingu kiasi, mvua na ngurumo katika maeneo machache na vipindi vya jua. “Matazamio kwa siku ya Jumatatu Aprili 23, 2018, mvua inatarajiwa kupungua katika maeneo mengi ya nchi,” imesema…

Soma Zaidi >>

MBEYA CITY VS YANGA SC, HAPATOSHI SOKOINE MBEYA.

Jioni ya leo Jumapili April 22, 2018, macho na masikio ya wapenzi wa kabumbu nchini yatakuwa jijini Mbeya kwenye dimba la Sokoine, kushuhudia mtanange wa kukata na mundu baina ya timu ya soka ya Mbeya City ya jijini Mbeya na Yanga SC kutoka jiji la Dar es Salaam. Mtanange huo utapigwa majira ya saa kumi jioni, ambao unategemewa kuwa wa aina yake, kutokana na historia ya timu hizo mbili, hasa zinapokutana katika dimba la Sokoine. Mbeya City wamekuwa wakiwasumbua sana Yanga wanapokutana katika dimba hilo, ambalo mara nyingi Yanga wamekuwa…

Soma Zaidi >>