MAHAKAMA YA  KISUTU YAPIGA DANADANA KUSOMWA MAELEZO YA AWALI VIGOGO TFF

MAHAKAMA ya Hakimu Mkazi Kisutu imesogeza mbele tarehe ya  kuwasomea maelezo ya awali (PH ) ya vigogo watatu wa Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) hadi Aprili 18/2018. Hatua hiyo imekuja baada ya Wakili wa Serikali, Shedrack Kimaro kuitaarifu Mahakama kuwa wanaomba kufanya mabadiliko ya hati ya mashtaka kwanza ndiyo waendelee na PH. Wakili Kimaro amedai, “kesi leo imepangwa kwa ajili ya PH, Mimi ndiyo nimepangiwa kuendelea na kesi hii, nimefanya Mawasiliano na (Takukuru) tukapitia ushahidi uliokusanywa hivyo tunaomba kufanya mabadiliko ya hati ya mashtaka Kwa kuongeza washtakiwa wengine…

Soma Zaidi >>

AJALI YA NDEGE YAUA WATU 257

Wizara ya Ulinzi nchini Algeria imesema takriban watu 257 wamefariki dunia baada ya ndege ya kijeshi kuanguka kaskazini mwa nchi hiyo. Kisa hicho kilitokea muda mfupi baada ya ndege hiyo kupaa kutoka uwanja wa ndege wa kijeshi wa Boufariki karibu na mji mkuu wa Algiers asubuhi. Wengi wa waliouawa ni wanajeshi na familia zao kulingana na wizara ya ulinzi huku wafanyakazi 10 wa ndege hiyo pia wakifariki. Haijulikani ni nini haswa chanzo cha kuanguka kwa ndege hiyo. Afisa mkuu wa jeshi ameagiza uchunguzi wa ndege hiyo na atatembelea eneo la…

Soma Zaidi >>

UKOSEFU WA ELIMU YA BARABARANI HUCHANGIA ONGEZEKO LA AJALI

Imeelezwa kuwa ukosefu wa elimu ya barabarani usalama barabarani ni moja ya sababu zinazochangia kutokea kwa ajali za barabara mkoani Ruvuma, Akizungumza katika mkutano uliowahusisha mkuu wa mkoa wa Ruvuma, Christina Mndema, TARURA, TANROAD  na wamiliki wa vyombo vya moto mkoani humu Kamanda wa polisi  Gemini Mushi  amebainisha sababu zinazochangia kutokea kwa ajali mkoani humo, Aliziainisha sababu hizi ni pamoja na Uchakavu wa vyombo vya usafili, unosefu wa umakini kwa madereva, Madereva kutumia vilevi na starehe zinazowachosha wakiwa njiani, Madereva kufanya kazi kwa mda mrefu bila kupumzika,malipo hafufu kwa madereva,…

Soma Zaidi >>

SHIRIKA LA UNHCR LAANZA KUWARUDISHA NYUMBANI WAKIMBIZI WA AFRIKA YA KATI KUTOKA NCHINI KONGO(BRAZZAVILE)

Wakimbizi kutoka Jamhuri ya Afrika ya Kati waliokuwa wakiishi Betou, sehemu ya kaskazini mwa Jamhuri ya Kongo (Brazzaville) wameanza kurudishwa nyumbani. Wanatumia faida ya mpango wa kurudi kwa hiari na shirika la wakimbizi la Umoja wa Mataifa, (UNHCR) lililotangaza mwezi Machi mwaka huu. Huu mpango ni pamoja na wakimbizi wengine wapatao 6,000 waliokuwa wakiishi kambi ambayo ipo kilomita 50 kutoka mpaka wa nchi yao. Sebastian Sangba, mmoja wa wakimbizi alikuwa kati ya kundi la kwanza la wakimbizi 100 walirudi nyumbani alisema, “Chochote utakacho unaweza kupata lakini mtu hujihisi vizuri akiwa…

Soma Zaidi >>

RAIS MAGUFULI ATEUA MWENYEKITI BODI YA TAIFA YA WAHASIBU

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Magufuli amemteua Prof. Isaya Jayambo Jairo kuwa Mwenyekiti wa Bodi ya Taifa ya Wahasibu na Wakaguzi wa Hesabu (NBAA). Taarifa iliyotolewa na Katibu Mkuu Kiongozi Balozi John Kijazi imeeleza kuwa uteuzi wa Prof. Jairo unaanza leo April 11, 2018. Prof. Jairo ni Mkuu wa Chuo cha Kodi (ITA) na ameteuliwa kushika wadhifa huo kwa kipindi cha pili baada ya kipindi chake cha kwanza kumalizika.    

Soma Zaidi >>

MAZINGIRA MAZURI YA UWEKEZAJI YAWAVUTIA WAWEKEZAJI UFARANSA, WAAHIDI KUWEKEZA NCHINI

Chama cha Waajiri nchini Ufaransa-MEDEF kinachowakilisha asilimia 75 ya sekta binafsi nchini humo, chenye kampuni wanachama takribani 750,000, kwa kushirikiana na Taasisi ya Sekta Binafsi nchini-TPSF, Ubalozi wa Tanzania Paris na Ubalozi wa Ufaransa Dar es Salaam. Kimeandaa  Jukwaa la Kimataifa la Biashara linalojulikana kwa jina la TPSF-MEDEF International Business Forum, litafanyika Jumatano ya Aprili 18 mwaka huuu katika Hoteli ya Serena iliyoko Jijini Dar es Salaam. Jukwaa hilo litatanguliwa na ujio wa Ujumbe wa viongozi wa wafanyabiashara kutoka nchini Ufaransa utakaotembelea Tanzania kwa muda wa siku tatu kuanzia Aprili…

Soma Zaidi >>

MAHAKAMA YAKASIRISHWA NA KITENDO CHA JAMHURI KUTOTEKELEZA AMRI ZAKE

Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu imeuvaa upande wa mashtaka kutokana na kushindwa kutekeleza amri yake ya kumpeleka mmiliki wa IPTL, Harbinder Sethi kutibiwa katika Hospitali ya Taifa Muhimbili. Kufuatia kutotekelezwa kwa amri hiyo, Hakimu Mkazi Mkuu wa Mahakama ya Kisutu, Huruma Shaidi, amevitaka vyombo husika kuheshimu amri zinazotolewa na mahakama ikiwemo kuziekeleza. Hakimu Shaidi amesema haipendezi Mahakama kila wakati kutoa amri ambzo hazitekelezwi, na kuamuru tena Mshtakiwa Sethi kupelekwa hospitali kabla hajatoa amri nyingine kwa mujibu wa sheria. Awali, Wakili wa serikali, Nassoro Katuga amedai upelelezi wa kesi hiyo haujakamilika,…

Soma Zaidi >>

WAFUNGWA WA KISIASA WAACHIWA HURU SUDAN

Rais wa sudan, Omar Al-Bashir ameagiza kuachiwa huru kwa wafungwa wote wa kisiasa  nchini humo na kusema wakati wa kushughulikia masuala ya kisiasa  sasa umefika. Uamuzi huo umekuja  baada ya vyama vya kisiasa na makundi ya asasi za kiraia nchini humo kushiriki mijadala ya kitaifa inayoendelea ikihusisha wawakilishi wa serikali alipohutubia wabunge ambao waanaza muhula mpya wa vikao vya bunge na kuwataka wanasiasa  wanasiasa kufahamu kuwa hiki ni kipindi cha mabadiliko ya kisiasa nahivyo serikali itafanya kila liwezekanalo kutimiza lengo lake. “kuachiwa wafungwa wote wa kisiasa ni juhudi za umoja…

Soma Zaidi >>

RC MAKONDA AWATOLEA NJE VIGOGO WANAOMTAFUTA KWA SIRI KUFICHA SKENDO YA KUTELEKEZA WATOTO

Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda amedai kuwa hadi sasa kuna vigogo takribani 107 waliotajwa kwenye skendo ya kutelekeza watoto, huku akiwanyooshea kidolea baadhi yao wanaotaka kuonana naye kwa siri kuwa hana nafasi hiyo. Akizungumza na kina mama waliojitokeza kupeleka malalamiko yao ofisini kwake, Makonda amesema kuanzia kesho waliotajwa kutelekeza watoto wataanza kupelekewa barua za wito, huku akisisitiza watakaokaidi wito huo watachukuliwa hatua kali za kisheria. Aidha, Makonda amesema wadau mbalimbali wamejitokeza kuwasaidia watoto wanaodaiwa kutelekezwa na baba zao ikiwemo kuwalipia bima za afya ili waweze kumudu…

Soma Zaidi >>

ZIMBABWE KURUHUSU WAANGILIZI WA KIMATAIFA WA UCHAGUZI KUFUATILIA KATIKA UCHAGUZI UJAO BAADA YA MIAKA 15

Tume yenye mamlaka ya uchaguzi Nchini Zimbabwe, imesema itaruhusu waangalizi wa kimataifa kutoka nchi za magharibi kufuatilia uchaguzi wake kwa kwanza baada ya miaka zaidi 15. Hapo jana jumanne tarehe 10 aprili 2018, hati rasmi za taratibu za uchaguzi huo unaotegemewa kufanyika mwezi july mwaka huu, zilionyesha kufuta zuio lililokuwa limepiga marufuku na kiongozi wa zamani Robert Mugabe. Hii hatua ni ya kwanza, na inayoonyesha utawala wa wenye sifa za kidemokrasia kwa Rais wa sasa Emmerson Mnangagwa tangu alipokuwa na mamlaka kuongoza nchi hii mnamo Novemba mwaka jana, baada ya…

Soma Zaidi >>