Johari akiri kuwa soko la Bongo Movie halisomeki.

Msanii wa filamu za kibongo nchini almaarufu kama BONGO MOVIE, Blandina Chagula ( Johari) ameiambia Darmpya.com kuwa soko la filamu zao kwasasa hapa Tanzania imekuwa mbaya na kukatisha tamaa. “Soko letu la filamu hapa nchini limepoteza mvuto sana hasa kutokana na wapenzi wa filamu hizi kupungua na pia hata kwa movie mpya zinazotoka soko lake limekuwa gumu sana kutokana na CD za ku copy na kukodisha kuwa nikitu cha kawaida kilicho zoeleka sana mitaani kwa sasa. Kiukweli sanaa yetu inakatisha tamaa na inahitaji sana kunusuriwa.” Alisema . Akizungumzia project yake…

Soma Zaidi >>

ACT yaikumbusha serikali kutoa taariza uchunguzi wa tukio la Lissu, kupotea mwandishi wa Mwananchi

  Chama cha ACT-Wazalendo kimeitaka serikali kutoa taarifa ya uchunguzi wa kupotea kwa Mwaandishi wa gazeti la Mwananchi, Azory Gwanda na wa tukio la kushambuliwa risasi na watu wasiojulikana, Mbunge wa Singida Mashariki, Tundu Lissu. Wito huo umetolewa leo jijini Dar es Salaam na Katibu wa Itikadi na Uenezi, Ado Shaibu wakati akizungumza na wanahabari ambapo amesema matukio hayo hayawezi kuachwa kwani madhara yake ni makubwa. “Matukio haya hayawezi kuachwa hivi hivi tu kwani madhara yake ni makubwa sana kwa usalama wa nchi yetu na raia wake. Serikali pia imalize…

Soma Zaidi >>

Dubai yazindua jengo refu zaidi duniani lenye ghorofa 75

Jana Jumapili Februari 11, 2018 Dubai iliendeleza desturi yake ya kuwa na majengo marefu zaidi duniani, kwa kuzindua jengo lingine la Gevora Hotel Towers. Jengo hilo linakuwa la kwanza duniani kwa urefu kutokana na kuwa na ghorofa 75 na urefu wa mita 356 kwenda juu. Hata hivyo, rekodi ya jengo refu la hoteli duniani ilikuwa inashikiliwa na Dubai yenyewe ambapo jengo la hoteli la JW Mariott Marquis ambalo limezidiwa mita moja tu na jengo jipya la Genova Hotel ndio lilikuwa linashikilia rekodi hiyo.

Soma Zaidi >>

ACT yakosoa taarifa ya Serikali kuhusu uchumi, utawala bora

Chama cha ACT-Wazalendo kimeikosoa taarifa ya Msemaji wa Serikali, Dkt. Hassan Abass iliyoonesha kuimarika kwa ukuaji uchumi na utawala bora hapa nchini. Akizungumza na wanahabari leo jijini Dar es Salaam, Katibu wa Itikadi na Uenezi ACT-Wazalendo, Ado Shaibu, amedai kuwa katika taarifa hiyo, Dkt. Abass alikwepa kueleza maudhui yaliyoibuliwa kwenye matokeo ya ripoti ya Jarida la The Economist, aliyotumia katika kuonesha uimarikaji wa hali ya utawala bora nchini. Amedai kuwa, ukweli uliowekwa wazi kwenye ripoti hiyo unaonyesha Tanzania kushuka kutoka alama 5.76 iliyokuwa mwaka 2016 hadi 5.47 mwaka 2017, pia…

Soma Zaidi >>

RC Mnyeti asema hawezi kutoa msaada wa kiserikali kwa Madiwani Chadema kutekeleza ahadi zao

Mkuu wa Mkoa wa Manyara, Alexander Mnyeti amesema yupo tayari kupokea simu ya diwani wa CCM hata ikiwa usiku wa manane ili kumpa msaada. Mnyeti aliyasema hayo jana katika mkutano wa hadhara kwenye kata ya Haydom wilayani Mbulu, ambapo aliwataka madiwani wa Chadema kuhamia CCM kutokana kwamba hawezi kuwapa msaada wakiwa ndani ya chama hicho cha upinzani. Amewataka madiwani hao kujiunga na CCM ili ashirikiane nao katika kutekeleza ilani ya uchaguzi ya chama tawala. Alidai kuwa, diwani wa Chadema haiwezi kufanikisha maendeleo ya wananchi kwa kuwa hakuna atakayemsikiliza akkiwasilisha hoja…

Soma Zaidi >>

Marekani yajitoa katika mazungumzo ya Israel na Palestina kuhusu Mji wa Yerusalem

Marekani yajitoa katika mazungumzo ya utafutaji wa suluhu ya mgogoro unaokabili mataifa mawili ya Palestina na Israeli kuhusu mmiliki halali wa mji wa Yerusalemu. Rais wa Marekani, Donald Trump aliwaambia waandishi wa habari kwamba serikali yake haina tena cha kuzungumza zaidi juu ya mgogoro huo. Alisema suala la Yerusalem limetoka kwenye meza ya mazungumzo baada ya uamuzi wake wa kutangaza mji huo kama mji mkuu wa Israel na kuhamisha ubalozi Marekani kutoka mji wa Tel Aviv. Uamuzi wa Trump juu ya kuutambua Yerusalemu kama mji mkuu wa Israeli ulivunja sera…

Soma Zaidi >>

Uwanja wa Ndege London wafungwa baada ya bomu kuonekana

Uwanja wa Ndege wa London umefungwa baada ya bomu la vita vya pili vya dunia kupatikana kwenye mto ulio karibu wa Thames. Uwanja huo utafungwa siku nzima n azote za ndege zimefuntwa kitendo kilichoathiri abiria takribani 16,000. Bomu hilo liligunduliwa jana Jumapili eneo la George V wakati wa shughuli za kikazi mashariki mwa mji wa London. Polisi waliufunga uwanja huo na kusema kuwa, wanashirikiana na Jeshi la Wanamaji kuondoa bomu hilo.

Soma Zaidi >>

Marekani yabadili msimamo wake kuhusu Korea Kaskazini, yataka mazungumzo

Nchi ya Marekani imesema iko tayari kufanya mazungumzo na Korea Kaskazini bila ya kuwepo masharti yoyote. Kauli hiyo imetolewa na Makamu wa Rais Marekani, Mike Pence ambapo aliliambia gazeti la The Washington Post kuwa, kama Korea Kaskazini inataka mazungumzo, utawala wa Rais wan chi hiyo, Donald Trump utafanya hivyo. Hata hivyo, aPence amesema vikwazo vitaendlea kuwepo hadi pale Korea Kaskazini itakapochukua hatua za kumaliza mpango wake wa silaha za nyuklia. Awali, utawala wa Trump ulisema hautafanya mazungumzo na Kiongozi wa Korea Kaskazini Kim Jong-un hadi pale atakapo kuwa tayari kuachana…

Soma Zaidi >>

IGP Sirro amuapisha Kamishna wa Polizi Zanzibar

Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini, IGP Simon Sirro mapema leo Februari 12, 2018 amemuapisha Kmishna wa Polisi, CP Mohamed Hassani Haji kuwa Kamishna wa Polisi Zanzibar. Hafla hiyo imefanyika Makao Makuu ya Jeshi la Polisi nchini yaliyopo jijini Dar es Salaam na kuhudhuriwa na Makamishna na Maofisa Wakuu Waandamizi wa Jeshi la Polisi kutoka Tanzania Bara na Zanzibar. Baada ya kula kiapo cha utii mbele ya IGP Sirro, CP Haji pia alikula kiapo cha Maadili ya Uongozi wa Umma  mbele ya Katibu wa Viongozi wa Utumishi wa Umma, John…

Soma Zaidi >>

IGP Sirro atoa maagizo mazito kwa Kamishna wa Polisi Zanzibar

Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini, IGP Simon Sirro leo Februari 12, 2018 amemtaka Kamishna wa Polisi Zanzibar, CP Mohammed Hassani Haji kushughulikia matukio yenye viashiria vya ugaidi, rushwa, dawa za kulevya na utovu wa nidhamu kwa Maafisa Polisi na askari. IGP Sirro ametoa maagizo hayo leo jijini Dar es Salaam, baada ya kumuapisha CP Haji kuwa Kamishna wa Polisi Zanzibar. “Viashiria vya ugaidi maana yake, kuna matukio kwa ndani ukiangalia kuna muelekeo wa ugaidi, unyang’anyi kwa kutumia sialaha kama ujambazi kama viashiria, ili tatizo ni la dunia nzima, kwa…

Soma Zaidi >>