CCM KWA ALIMAUA WAMPOKEA RASMI SAID MTULIA

Chama Cha Mapinduzi (CCM) tawi la Alimaua A Kata ya Kijitonyama, Jijini Dar es Salaam, kimempokea na kumpa kadi ya uwanachama Ndg Said Mtulya aliyekua Mbunge wa Kinondoni kwa tiketi ya CUF. Hafla hiyo fupi iliandalia na uongozi wa CCM tawini hapo wakiongozwa na Mwenyekiti  Kassim Sultani Ngonwe, Katibu Juma Mkorogo Juma na Katibu Mwenezi Bi Emily Sanga. Pia uongozi wa tawi uliwaalika uongozi wa Kata ya Kijitonyama na wilaya ya Kinondoni. Katika Hafla hiyo Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi ( CCM) tawi la Alimaua A aliendesha zoezi la kumkabidhi…

Soma Zaidi >>

TANZANIA NA RWANDA ZAKUTANA KUSAINI MAKUBALIANO KUKOMESHA UHALIFU

Wakuu wa Polisi wa nchi za Tanzania na Rwanda, wamekutana kusaini makubaliano ya kufanya operesheni ya pamoja ya kukomesha uhalifu yaliyofikiwa mwaka 2012. Kikao hicho cha pamoja kilifanyika kati ya Inspekta Jenerali wa Polisi (IGP), Simon Sirro na Mkuu wa Jeshi la Polisi Rwanda, Emmanuel Casana kutathmini makubaliano hayo. Katika mazungumzo hayo Kamanda Sirro alisema kuwa, walisaini makubaliano ya kufanya operesheni kwa pamoja kukomesha uhalifu na kubadilishana watalaam. Alisema, kuna watalaam kutoka Rwanda watatoa mafunzo ya kushughulikia makosa kimtandao. Aidha alisema kuwa, Warwanda ni wazuri kwenye masuala ya kudhibiti uhalifu…

Soma Zaidi >>

KABEJI INAVYOTIBU VIDONDA VYA TUMBO

Kabeji ni nini? Kabeji ni aina ya mboga ya majani inayostawi kwa wingi Wilaya ya Lushoto Mkoani Tanga, mara nyingi watu hutumia kabeji kama mboga na wengine hulikatakata na kulitengeneza saladi (kachumbali). Ikumbukwe kuwa mbali na kabeji kutumika kama mboga lakini pia ni dawa nzuri ya Vidonda vya tumbo. Pamoja na Kabeji kuwa moja ya dawa bora za asili zinazoweza kutibu vodonda vya tumbo lakini pia Kabeji ina ‘lactic acid’ambayo husaidia kutengeneza amino asidi inayohamasisha utiririkaji wa damu kwenda kwenye kuta za tumbo jambo linalosaidia kuuongezea nguvu ukuta wa tumbo…

Soma Zaidi >>

CUF YABARIKI KUONDOKA KWA MTULYA, YAPINGA SABABU ZA KUONDOKA KWAKE

  Chama cha Wananchi (CUF) kimeridhia taarifa ya kujiuzuru kwa Mbunge wake wa Kinondoni Maulid Mtulya huku kikidai kutorishwa na sababu alizozitoa za kuondoka katika chama hicho. Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na CUF kwa Vyombo vya habari, zimeeleza kuwa Chama Cha Wananchi, kimepokea taarifa ya kujiuzuru uanachama kwa Mbunge huyo kupitia mitandao ya kijamii, Ubunge na nyadhifa nyingine alizokuwa nazo akiwa mwanachama wa CUF na wamemsikia akieleza sababu zake za kufanya maamuzi hayo. Aidha taarifa hiyo iliwajulisha wanachama wa CUF, na Watanzania kwa ujumla kwamba Maamuzi aliyoyafanya Maulid Mtulia…

Soma Zaidi >>

MHE.SAMIA: MSIWAFICHE WANAOWAFANYIA UOVU WALEMAVU ZANZIBAR

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan alimewataka wanafamilia kutoficha maovu wanayofanywa kwa watu wenye ulemavu na kwamba Serikali kwa nguvu zote. Makamu wa Rais aliyasema hayo wakati wa Maadhimisho ya Siku ya Watu wenye ulemavu duniani iliyofanyika Mkoa wa Kusini, Unguja, Zanzibar. Mhe. Samia alitoa rai kwa kusema kuwa, kila mmoja miongoni mwa jamii ni askari wa mwenzie katika kuhakikisha kuwa tunalinda haki na usawa wa watu wenye ulemavu na kwamba serikali inakemea vitendo vya ubakaji na udhalilishaji kwa watu wenye ulemavu. “Vitendo hivi…

Soma Zaidi >>

AISIIIII……..U KILL ME 01

Mwandishi: Eddazaria G.Msulwa (Next level Author) 0657072588   Kaubaridi kakali ka asubuhi kananifanya niwe ninabingirika bingirika, kwenye kitanda changu cha sita kwa sita. Sitamani kabisa kunyanyuka kwenye kitanda changu hichi, hii ni kutokana na uchovu unaosababishwa na pirika pirika zangu za siku tano za wiki, na hizi siku mbili za mapumziko muda mwingi ninazitumia kushinda chumbani kwangu. Kiupepo cha feni kinachonipiga kwa mwendo wa taratibu, kinazidi kuongezeka zaidi na kiupepo cha mvua mvua inayo nyesha huko nje. Taratibu naanza kulipapasa shuka langu sehemu lilipo na kujifunika vizuri mwilini mwangu. Kabla…

Soma Zaidi >>

YALIYOSEMWA NA ALIYEKUWA MBUNGE WA KINONDONI KUPITIA CUF MAULID MTULIA MARA BAADA YA KUKABIDHIWA KADI YA CCM LEO JUMATATU TAREHE 04/12/2017

“Nimejivua nyadhifa zangu zote ya Ubunge wa Kinondoni na vyeo vyote nilivyokuwa navyo CUF na kuamua kujiunga na CCM kutokana na kuridhishwa na CCM ya sasa na utendaji wa Rais Dk. Magufuli” – Mtulia “Mimi ni mgeni na salamu ninayoijua ya CCM ni CCM Oyeee” – Mtulia “Nimejiunga na CCM ili kuunga mkono kazi nzuri inayofanywa na Rais Dk. Magufuli” – Mtulia “Nimetoka kwenye chama chenye migogoro mingi, nimekuja kwenye chama chenye amani, haki na Demokrasia ya kweli” – Mtulia “Ningekuwa Mbunge kupitia CCM ningefanya mengi makubwa zaidi” – Mtulia…

Soma Zaidi >>

WANAFUNZI WA (UDSM) WASIMULIA SAKATA LA UFA LINAVYOWAPA HOFU

Baadhi ya wanafunzi wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (UDSM) wameingia hofu baada ya mabweni wanayoishi kuwa na nyufa. Mabweni hayo yanayotumiwa na wavulana katika jengo la Block A yana nyufa sehemu mbalimbali kuanzia chini hadi ghorofa ya tatu. Mbunge wa serikali ya wanafunzi (Daruso), Simon Masenga amesema nyufa hizo zilianza kuonekana wiki mbili zilizopita. Amesema walitoa taarifa kwa meneja wa hosteli lakini majibu waliyopewa ni kuwa majengo hayo yako chini ya Wakala wa Majengo Tanzania (TBA). Mbunge mwingine wa serikali ya wanafunzi, Kumbusho Dawson amesema leo Jumatatu Desemba…

Soma Zaidi >>

BUNDUKI YA JOSHUA NASSARI YASHIKILIWA KWA UCHUNGUZI

Wakati mbunge wa Arumeru Mashariki (Chadema), Joshua Nassari akilihusisha tukio la kuvamiwa nyumbani kwake na watu wasiojulikana na masuala ya kisiasa, polisi inashikilia bunduki ya mwanasiasa huyo kwa uchunguzi. Polisi mkoani Arusha imesema imeanza uchunguzi wa kina wa kuwasaka washukiwa, huku ikichunguza silaha ya Nassari aina ya shotgun, ikisema tukio hilo lina utata kutokana na mazingira lilivyotokea. Kamanda wa polisi wa mkoa, Charles Mkumbo amesema  kuwa wameanza uchunguzi wa kina ili kubaini endapo kulikuwa na tukio au la. “Tunaifanyia uchunguzi bunduki yake, tunataka kujiridhisha endapo kulikuwa na tukio au la,”…

Soma Zaidi >>

POLEPOLE: HATUMPOKEI MTU ANAYETAKA KUJA KWENYE CHAMA BILA KUFUATA TARATIBU

Katibu wa Itikadi na Uenezi wa Chama cha Mapinduzi (CCM), Humphrey Polepole amesema, Chama cha Mapinduzi (CCM) hakitampokea mtu yeyote anayetaka kurudi ndani ya chama hicho bila kufuata utaratibu. Kauli hiyo imekuja baada ya aliyekuwa Mbunge wa Jimbo la Kinondoni (CUF), Maulid Said Abdallah Mtulia kutangaza kujiuzulu nafasi zake zote za uongozi alizokuwa akizishikilia katika chama hicho na kutangaza kwenda CCM Polepole aliyasema hayo wakati akiwahutubia wananchi wa CCM Mkoa wa Mara katika uchaguzi wa Mwenyekiti wa Mkoa wa Chama. “Ameamua kule aliko haoni itikadi,haoni siasa, haoni mwelekeo, Chama kina…

Soma Zaidi >>