DR.SHIKA ATOA AHADI ZA MABILIONI KWENYE MAHAFALI KAHAMA

Dk Louis Shika ‘Bilionea’ aliyejizolea umaarufu baada ya kuibuka katika mnada wa kununua nyumba za mfanyabiashara Said Lugumi ametua mjini Kahama na kupokewa na watu wengi. Mapokezi ya Dk Shika aliyetua mjini hapa kuwa mgeni rasmi katika mahafali ya Chuo cha Afya cha Kahama (Kahama College of Health Science), yameongozwa na msururu wa magari zaidi ya 50 na kupita kwenye mitaa mbalimbali kabla ya kuelekea chuoni, Kata ya Mwendakulima, nje kidogo ya mji wa Kahama. Mapokezi hayo leo Alhamisi Novemba 23,2017 yameongozwa na Mkurugenzi wa chuo hicho, Yona Bakungile kuanzia…

Soma Zaidi >>

KAFULILA ATUHUMIWA NA MKEWE

Jesca Kishoya ambaye ni Mbunge wa Viti Maalum na mke wa aliyewahi kuwa Mbunge wa Kigoma Kusini, David Kafulila amesema sababu alizotoa mume wake za kuihama Chadema hazina mashiko. Jesca Kishoya amesema Kafulila ameingia katika kundi la wanasiasa wasiokuwa na msimamo. Kishoya amesema, David amekuwa na msimamo usioyumba lakini anashangazwa kwanini ameingia kwenye mtego huo mbovu. Mimi bado naamini Chadema ni mahala sahihi kabisa ambapo sijafikiria ipo siku nitatoka. David anasema Chadema sio mahali sahihi kuzungumzia ufisadi kwa sasa je huko CCM mafisadi wameisha? alihoji mke wa Kafulila.

Soma Zaidi >>

BODI YA LIGI KUU YATOA ADHABU KALI KWA VILABU VYA MPIRA WA MIGUU

Kamati ya Bodi ya Ligi Kuu ya Uendeshaji na Usimamizi wa Ligi katika kikao chake cha Novemba 22, 2017 ilipitia mwenendo na matukio mbalimbali ya Ligi kwa msimu wa 2017/2018 inayoendelea hivi sasa. Klabu ya Tanzania Prisons imepewa Onyo Kali kwa kuwakilishwa kwenye benchi na ofisa tofauti na yule aliyeudhuria kikao cha maandalizi (pre match meeting) cha mchezo kati yake na Kagera Sugar uliofanyika Novemba 4, 2017 kwenye Uwanja wa Kaitaba mjini Bukoba. Katika kikao hicho, Prisons iliwakilishwa na Meneja wake Erasto J. Ntabah lakini kwenye benchi alikaa Hassan Mtege.…

Soma Zaidi >>

DC GONDWE AWATAKA WANANCHI KUICHANGIA SEKTA YA AFYA

Mkuu wa Wilaya ya Handeni, Godwin Gondwe amewataka wananchi wa Kata ya Kwamgwe kuendelea kujitoa kikamilifu katika kuchangia shughuli za kijamii ili kuendana na kasi ya rais Dkt. John Magufuli katika kuleta maendeleo endelevu. Akizungumza na wakazi wa Kata ya Kwamgwe wakati akikabidhiwa zahanati iliyojengwa kwa hisani ya shirika la maendeleo la World Vision Tanzania, mkuu wa wilaya aliwaomba wananchi waendelee na moyo wa kujitolea katika kuchangia kazi za maendeleo ili kijiji kiweze kujikwamua. “Nawaomba ndugu zangu, sisi wote ni wanaKwamngwe, lazima tuamue kuchangua mambo muhimu matatu, kutambaa, kutembea au…

Soma Zaidi >>

TUNDU LISSU KUSAFIRISHWA KUPELEKWA AFRIKA KUSINI KWA MATIBABU

Mbunge wa Singida Mashariki (CHADEMA), Tundu Lissu anatarajiwa kusafirishwa nje ya nchi kwa matibabu mwezi mmoja kuanzia sasa. Kwa mujibu ya taarifa iliyotolewa na familia yake imeeleza kuwa, Lissu baada ya kupata matibabu nje ya nchi amepanga kufanya mambo matano akirejea salama . Akizungumza na Waandishi wa Habari leo Alhamisi Novemba 23, kaka wa Tundu Lissu, Wakili Alute Mughwai alisema, taratibu za kumsafirisha nje ya nchi zimeanza. Lissu, ambaye ni mjumbe wa Kamati Kuu na Mwanasheria Mkuu wa Chadema amelazwa katika Hospitali ya Nairobi nchini Kenya baada ya kushambuliwa kwa…

Soma Zaidi >>

WAZIRI WA ELIMU AMSIMAMISHA KAZI OFISA MIKOPO CHUO CHA ARDHI

Waziri wa Elimu, Profesa Joyce Ndalichako amemsimamisha kazi Ofisa Mikopo wa Chuo Kikuu Ardhi, Rajabu Kipango kwa madai ya kushindwa kukamilisha mchakato wa kutoa mikopo kwa wanafunzi waliopatiwa mkopo licha ya serikali kuwasilisha fedha hizo kwa wakati. Hatua hiyo ya kusimamishwa kazi kwa Ofisa huyo, ni matokeo ya malalamiko ya mara kwa mara yanayotolewa na Wanafunzi wa Vyuo vya Elimu ya Juu nchini kuhusiana na kucheleweshewa mikopo licha ya serikali kufanya jitihada kutoa fedha hizo. Katika siku za hivi karibuni Serikali iliwahi kueeleza kwamba, matatizo ya Bodi ya Mikopo ya…

Soma Zaidi >>

WAZIRI INDIA AWAKERA WANANCHI KWA KUHUSISHA SARATANI NA DHAMBI

Raia nchini India wasikitishwa na kauli iliyotolewa na Waziri kutoka Jimbo la Assam la kusema kuwa, ugonjwa wa saratani ” ni haki ya kiimani ” inayosababishwa na  thambi mtu alizowahi kuzifanya. Waziri huyo Himanta Biswa Sarma ametoa kauli hiyo alipokuwa akizungumza kwenye tukio la umma katika eneo la Guwahati Jumatano na kusema kuwa watu pia wanaweza kupata ugonjwa kama saratani kutokana na dhambi walizotenda wazazi wao. Wagonjwa wa saratani na ndugu zao wamesema kuwa wamesikitishwa sana na kauli ya waziri huyo ambaye ni kiongozi mkubwa katika jamii yake. Vyama vya…

Soma Zaidi >>

RUGE: SERIKALI INAIKWAMISHA FIESTA

Mkurugenzi Uzalishaji na vipindi wa Clouds Media Group Ruge Mutahaba, amesema anasikitika kuona jinsi namna serikali inavyoiwekea vikwazo katika kufanikisha tukio la Fiesta litakalofanyika kwenye viwanja vya Leaders Novemba 25, 2017  Jijini Dar es salaam. Ruge ameyasema hayo katika kipindi cha 360 kinachorushwa na Cloue Tv wakati akielezea maandalizi ya tamasha la Fiesta litakalofanyika  Jijini Dar es salaam. Katika mahojiano hayo Ruge ameanza kwa kuwashukuru wale wote ambao wamewafariji baada ya ajali ya moto kutokea kwenye ofisi zao na kusisitiza moto hauwezi kuwarudisha nyuma katika maandalizi yao ya tamasha hilo.…

Soma Zaidi >>

KITUNGUU SWAUMU HUTIBU MAGONJWA 30

Kitunguu swaumu ni nini? Ni moja ya mmea ambao umependelewa sana na Mungu kwakuwa na viinilishe vingi na muhimu sana kwa afya ya binadamu. Mbali ya kutumika kama kiungo katika chakula ili kuleta ladha nzuri kwa mlaji, Kitunguu swaumu kinatibu magonjwa mengi karibu 30. Kitunguu swaumu ni jamii ya vitunguu ambayo kwa kitaalamu huitwa Allium sativum. Watu wa mabara mbali mbali duniani, walianza kutumia Kitunguu swaumu kama viungo katika mboga na tiba takribani  miaka 6000 iliyopita. Kitunguu swaumu kimetajwa kwenye vitabu mbalimbali vya dini vikielezea faida zake katika kutibu maradhi…

Soma Zaidi >>