AJINYONGA KWA UGUMU WA MAISHA NA KUACHA UJUMBE MZITO.


Na Allawi Kaboyo – Bukoba.

Mtu mmoja mkazi wa Kashai Manispaa ya Bukoba Mkoani Kagera, amekutwa amejinyonga kwa kamba ya katani hadi kufa Nyumbani Kwake kwa kile kinachodaiwa kuwa ni Kutokana na Hali ngumu ya Maisha baada ya kugundulika anaishi na Virusi vya Ukimwi.

Marehemu huyo aliyetambulika kwa jina la SALVATORY RWEYEMAMU (47) amegundulika akiwa amefariki katika Chumba chake alichokuwa akiishi katika Nyumba ya Bi. TAUS ALLY (mwenye Nyumba), Mnamo tarehe 6 Januari,2019 Majira ya Saa tatu Asubuhi mara baada ya Kijana wa Kaka ake (jina halikupatikana) alipokwenda kumjulia hali.

Imeelezwa na Majirani wa Marehemu kuwa, mara baada ya kijana huyo kufika nyumbani kwa marehemu Salvatory, alibisha hodi kwa muda mrefu bila kujibiwa, na hapo ikabidi kuulizia taarifa zake kwa majirani, hali hiyo ya sintofahamu ikapelekea Majirani hao pamoja na Rafiki wa Marehemu huyo Ndg, Andrew John kuchukua jukumu la kuchungulia dirishani ndipo walipogundua kuwa Bwana Salvatory mwili wake ulikuwa ukininginia Juu ya dari akiwa tayari amekwisha fariki.

Kutokana na hali hiyo taarifa zilitolewa kwa Mwenyekiti wa Kijiji Bw. VICTOR HERMAN na kufika eneo la Tukio mara moja kisha nae akalijulisha Jeshi la Polisi ambapo baada Polisi kuwasili eneo la tukio, ndipo waliutermsha Mwili wa Marehemu kutoka katika Kitanzi na katika kupekua pekua ndani wakakutana na Ujumbe Ulioachwa na Marehemu ukisomeka kuwa “Nimeamua kujiua maisha yamekuwa magumu, Ukimwi noma, baiskeli yangu ipo kwa fundi wapewe wanangu”

Kwa upande wake Mdogo wa marehemu BERNADETHA RWEYEMAMU (30) kwa masikitiko makubwa akisimulia kuhusu msiba wa marehemu kaka yake amesema kuwa, kwa wiki tatu zilizopita Marehemu alikuwa akijihisi kuumwa mara kwa mara, na baada ya kupimwa aligundulika kuwa ni muathirika wa VVU, hali iliyomfanya aanze kuzorota kiafya na kuwa mtu wa mawazo sana. Kwa kipindi chote hicho hadi umauti unamfika Marehemu Salvatory alikuwa akiishi peke ake na akiendelea na shughuli zake za kila siku za uchomeleaji vyuma, huku Dada mtu akipata muda wa kwenda kumsabahi pale ilipobidi.

Kutokana na Kifo hicho baadhi ya Marafiki na Jirani wa Marehemu ahawakusita kuzungumzia tukio hilo huku Bwana Andrew John akidai kuwa Marehemu alikuwa rafiki yake na Wakifanya shghuli zao pamoja katika karakana yao ya Uchomeleaj, na Kwa mara ya mwisho waliachana Juzi Akiwa katika hali ya kawaida kama siku zote japo alionekana Mwenye mawazo sana.

Nae Ndg, Denice James (27) Jirani wa marehemu alipokuwa akiishi amenukuliwa akisema kuwa Marehemu Salvatory (Babu) alikuwa mtu wa kujifungia ndani mara kwa mara na wakati mwingine angeweza kujifungia kwa kipindi cha siku tatu bila Kutoka Nje, ingawaje aliishi kwa mahusiano mazuri yeye na mjiarni zake wengine.

Mwili wa marehemu umechukuliwa na jeshi la polisi ambapo mkuu wa upelelezi wilaya Bukoba amethibitisha kutokea kwa tukio hilo na tayari Umehifadhiwa chumba cha maiti Katika Hospitali ya Rufaa Bukoba ukingoja taratibu za Mazishi.

Marehemu ameacha Mke na watoto watatu huku akisisitiza Baiskeli yake ipo kwa fundi wapewe watoto wake.

Related posts

Leave a Comment

This site uses Akismet to reduce spam. Learn how your comment data is processed.