CHADEMA: TUNAMTAKA DC MJEMA KUSITISHA ZIARA YAKE JIMBO LA UKONGA

Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) Mkoa wa Ilala kimesema kinamtaka Mkuu wa Wilaya ya Ilala, Sophia Mjema kusitisha mara moja ziara yake anayofanya hivi sasa katika kata mbalimbali za jimbo la Ukonga. Katika taarifa iliotolewa na chama hicho imeeleza kuwa, ziara hiyo ina kila dalili ya kuanza kufanyia kampeni Chama cha Mapinduzi (CCM) kabla ya muda wa kampeni kuelekea uchaguzi mdogo wa ubunge kwenye Jimbo hilo utakaofanyika tarehe 16 Septemba 2018. Ratiba ya mchakato wa uchaguzi mdogo katika Jimbo la Ukonga imetolewa na Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC)…

Soma Zaidi >>

JESHI LA POLISI LATII AGIZO LA KUKAMATA WANAKIJIJI WOTE KIJIJI CHA NGOLE, MBEYA.

Tayari magari yaliyosheheni maaskari wa kutosha yametumwa katika Kijiji cha Ngole kilichopo kata ya Ilungu wilayani Mbeya kwaajili ya kuwakamata wanakijiji hao kutokana na kutuhumiwa kuharibu mradi wa maji katika kijiji jirani cha Msheye. Kwa mujibu wa shuhuda wetu aliyepo kijijini hapo amedai kuwepo kwa hofu kubwa miongoni mwa wananchi wa kijiji hicho. Kwa upande wake Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mbeya, Ulrich Matei, amenukuliwa na chombo kimoja cha habari nchini, akithibitisha kuwatuma askari wake kwaajili ya kutekeleza agizo la Mkuu wa Mkoa wa Mbeya, Albert Chalamila. Mapema siku ya…

Soma Zaidi >>

MAVUNDE AITAKA TUME YA USULUHISHI NA UAMUZI(CMA) KUTOCHELEWESHA MASHAURI

Naibu Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu-Kazi,Vijana na Ajira *Mh Anthony Peter Mavunde amewataka wasuluhishi wa Tume ya usuluhishi na uamuzi (CMA) kufanya kazi kwa  uadilifu na kumua mashuri kwa uharaka. Pia ameitaka  Tume hiyo, kufanya kazi zao kwa uweledi na kwa kuzingatia maadili katika utoaji wa haki na pia kuhakikisha wanatoa maamuzi kwa wakati pasipo ucheleweshaji ili kusaidia kuchochea maendeleo ya Uchumi wa Viwanda. Mavunde ameyasema hayo leo asubuhi katika Uwanjanwa Jamhuri-Morogoro wakati akihitimisha ratiba ya awali ya siku 3 ya mafunzo ya Wafanyakazi wa (CMA) kutoka nchi…

Soma Zaidi >>

DC MJEMA AWATAKA WAFUGAJI KUFUATA SHERIA

Na Fatma Ally Mkuu wa Wilaya ya Ilala Sophia Mjema amewataka wananchi wa Ukonga kufuata sheria na taratibu za ufugaji wa Mifugo wa Mjini ili kuepusha adha inayowakumbuka wananchi pindi Mifugo hiyo inapokatisha barabarani. Agizo hilo amelitoa Leo jijini Dar es Salaam, wakati wa ziara yake ya kusikiliza kero za wananchi na kuzipatia ufumbuzi katika maeneo ya Ukonga, baada ya wananchi kutoa kero hiyo inayowasumbua kwa muda mrefu sasa. “Nimewasikia nataka ni waambie hili ni jiji huwezi kuwa na Mifugo ikawa inakatisha tu barabara lazima Mfugaji afuate sheria na sheria…

Soma Zaidi >>

IGP SIRRO:TUNAFANYA UCHUNGUZI UPELELEZI UKIKAMILIKA MBISE ATAFUNGULIWA MASHTAKA

Mkuu wa jeshi la polisi nchini IGP Simon Sirro amesema mwandishi wa habari Silas Mbise aliyedaiwa kupigwa na jeshi la polisi wiki iliyopita katika uwanja wa Taifa kwenye tamasha lililoandaliwa na klabu ya soka ya Simba alimkaba askari polisi na kuanza kumtishia. Hali hiyo imetokana baada ya polisi kumkataza mwandishi huyo kuingia kwenye eneo ambalo askari walisema Silas Mbise hakuwa anaruhusiwa kuingia. Aidha IGP Sirro amesisitiza kuwa polisi wanafanya uchunguzi wa tukio hilo na ulikamilika mwandishi huyo atafunguliwa mashtaka na atafikishwa kwenye vyombo vya sheria. Pia amesema, jeshi hilo linachunguza…

Soma Zaidi >>

RAIS TRUMP AAMURU AFISA USALAMA KUONDOLEWA ULINZI

Rais wa Marekani Donald Trump ameamuru kuondolewa ulinzi aliyekuwa mkuu wa shirika la ujasusi la Marekani ‘CIA’, John Brennan, kutokana na kile kinachodaiwa ni mtu asieaminika katika uadilifu na asiefuata misingi ya kazi yake katika siku za hivi karibuni. Kwa mujibu wa BBC, agizo la Trump limekuja ikiwa ni siku chache tu toka Brennan akaririwe akikosoa mkutano wa Trump na Rais wa Urusi Vladimir Putin uliofanyika mwezi Julai  katika mji wa Helsinki nchini Urusi. Brennan amepinga vikali agizo la Trump ambapo kupitia ukurasa wake wa Twitter amesema kuwa hatua hiyo ni mwendelezo…

Soma Zaidi >>

MLIPUKO WA BOMU WAUA 48 NA KUJERUHI 67, WAKIWEMO WANAFUNZI WA CHUO KIKUU

Watu 48 wanaripotiwa kupoteza maisha huku wengine 68 wakijeruhiwa vibaya kufuatia mlipuko wa bomu uliotokea katika kituo kimoja cha masomo ya ziada mjini Kabul nchini Afghanstan. Tukio hilo limetokea mapema  jana ambapo polisi wamesema mwanamme mmoja aliyekuwa amejifunga mabomu hayo alifika katika kituo hicho cha elimu huko magharibi mwa Afghanstan na kujilipua katikati ya wanafunzi waliokuwepo eneo hilo. Kundi la wapiganaji wa Talban limekanusha kuhusika na shambulio hilo, licha ya kushutumiwa kutokana na kawaida yake ya kuwashambulia waumini wa Kishia ambao wengi wanapatikana katika eneo hilo ambapo washia  wanaonekana kama wapiganani…

Soma Zaidi >>

WAZIRI UMMY MWALIMU ALETA NEEMA TANZANIA BAADA KWENDA ZIARA NCHINI CHINA

Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Ummy Mwalimu, amekutana na na Waziri wa Afya wa China na kukubaliana kuunda Kamati Maalumu ya kuratibu utekelezaji wa maeneo mapya ya ushirikiano katika tiba, mafunzo na utafiti. Waziri Mwalimu ambaye yuko nchini China katika ziara yake ya kikazi baada ya kupata mwaliko wa Waziri wa Afya, Ma Xiaowei, leo Agosti 15, 2018 ameendelea na ziara yake ambapo viongozi hao wamesaini makubaliana ya kuanzisha ushirikiano kati ya wizara zao katika sekta ya Afya. Makubaliano hayo yanajumuisha ushirikiano katika Tiba, Utafiti…

Soma Zaidi >>